HEADER AD

HEADER AD

CHADEMA YASEMA ITAENDELEA KUANDAMANA MPAKA SERIKALI ITAKAPOTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI

>> Mbowe awaambia wanakagera hawatachoka kuandamana

>>Wakerwa na mfumko wa bei ya Vyakula,

>>Wasisitiza Tume huru ya uchaguzi, Katiba Mpya

Na Alodia Babara, Bukoba

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kimefanya maandamano ya amani yaliyolenga kuishinikiza serikali kurekebisha mambo mbalimbali likiwemo suala la mfumko wa bei.

Maandamano hayo yamefanyika Aprili, 22, 2024, mkoani Kagera katika wilaya ya Bukoba, yaliyowahusisha wanachama wa Chadema pamoja na viongozi ngazi mbalimbali kuanzia Taifa hadi mitaa.

       Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA pomoja na wanachama  wao wakiwa kwenye maandamano.

Wanachama na wafuasi wa chama hicho wametembea kwa miguu takribani kilomita nne kuanzia mtaa wa Mafumbo kata ya Kashai hadi uwanja wa Mashujaa maarufu kama Mayunga kata ya Bilele 
na kufanya mkutano wa hadhara.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amesema hakuna jambo linaloweza kuongeza hisia na mtazamo zaidi ya maandamano.

Amesema kwamba maandamano siyo jambo la mzaha kwa sababu sio kila Chama cha siasa kinaweza kufanya maandamano maana maandamano ni ushawishi na ni turufu ya Chadema.



Aidha ametaja lengo la maandamano hayo kuwa ni kuitaka serikali irekebishe mambo mbalimbali ndani ya serikali huku mabango yaliyobebwa na wafuasi wa chama hicho yakiwa yameandikwa jumbe mbalimbali.

Jumbe hizo katika mabango ni pamoja na mfumuko wa bei za vyakula twafa" "bila haki hakuna amani" "Tunataka katiba mpya na tume huru ya uchaguzi" pamoja na mabango mengine mengi ambayo yalikuwa yanataka kupewa haki ambazo wamedhulumiwa.

Amesema maandamano hayo yataendelea ndani ya Kanda ya Ziwa Victoria katika wilaya nyingine pamoja na Taifa kwa ujumla mpaka pale serikali itakapofanyia kazi changamoto za wananchi.

No comments