HEADER AD

HEADER AD

MWANDISHI MKONGWE WA VITABU KUWA MGENI RASMI TUZO YA UANDISHI BUNIFU

Na Andrew Chale, Dar es Salaam

MWANDISHI Mkongwe wa vitabu Prof. Abdulrazak Gurnah anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika usiku wa tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu.

Tuzo hiyo itafanyika Aprili 13, 2024 katika ukumbi wa "The Super Dome" Masaki Jijini Dar es Salaam ambayo ni siku ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

      Prof. Abdulrazak Gurnah akisalimiana na viongozi 

Tuzo hizo kwa mwaka huu ni za msimu wa pili huku zikiwa zinaratibiwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) chini ya uangalizi wa Wizara ya Elimu. 

Akizungumza katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Prof. Gurnah ameeleza "  Hii heshima kubwa kualikwa kuja kuungana katika sherehe hii ya tuzo ya Nyerere ili kuwasaidia waandishi wenzangu.’’ Amesema Prof. Gurnah.

      Prof. Abdulrazak Gurnah Akizungumza na Waandishi wa habari 

Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda wakati akimpokea mgeni huyo amemshukuru Prof. Gurnah kwa kukubalia mwaliko huo kwani ni heshima ya kipekee kwa washiriki  wabunifu wa tuzo hizo kukutana na mwandishi huyo nguli.

Aidha katika tukio hilo la mapokezi, Waziri wa Elimu Prof. Mkenda aliambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba na wafanyakazi wa TET na wadau mbalimbali.

  Prof .Abdulrazak Gurnah akiteta jambo na wenyeji wake kushoto Waziri wa Elimu Prof Adolf Mkenda na kulia ,Mkurugenzi wa TET,Dkt Aneth Komba 

No comments