HEADER AD

HEADER AD

NGORONGORO YAZINDUA ZOEZI LA UPIGAJI KURA TUZO YA KIVUTIO BORA CHA UTALII AFRIKA

Na Mwandishi wetu, Arusha

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imezindua zoezi  la upigaji kura kuwania tuzo ya kivutio bora cha utalii barani Afrika kwa mwaka 2024 katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Jengo la Ngorongoro Jijini Arusha.

Akizindua kampeni hiyo ya upigaji kura kaimu kamishna wa Uhifadhi NCAA Victoria Shayo amesema zoezi hilo litachukua siku 131 kuanzia mwezi huu wa aprili na linatarajiwa kukamilika mwezi Septemba 2024.

Amesema eneo la hifadhi ya Ngorongoro mwaka jana lilifanikiwa kushinda tuzo hiyo inayoandaliwa na mtandao wa World travel Awards baada ya kushinda katika kinyang’anyiro hicho kilichohusisha vivutio .

"Vivuto vingine vya Table Mountain, Harbeestpoort aerial cableway, V & A Waterfront, Ruben Island vya Afrika kusini, ziwa Malawi, Okavango Delta ya Botswana, Pyramids of Giza ya Misri pamoja na hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro hali iliyoitangaza nchi yetu na kuongeza idadi ya watalii.

Kamishna Shayo amesema tuzo hizo zina umuhimu mkubwa katika kuendeleza sekta ya utalii nchini na duniani kwa ujumla na kutoa wito kwa watanzania na wageni wote wanaotembelea Tanzania kuipiga kura nyingi Ngorongoro ili kuiwezesha Ngorongoro kutetea taji lake.

Katika mwaka huu wa 2024 jumla ya Nchi tano barani Afrika za tuzo hiyo ambazo ni Tanzania, Afrika Kusini, Botswana, Misri na Malawi zinawania tuzo hiyo.

     Baadhi ya Viongozi wa NCAA wakionesha tuzo ambayo eneo la Hifadhi ya Ngorongoro lilishinda nwaka jana kama kivutio bora cha utalii barani Afrika.

"Wapigaji kura duniani kote watatakiwa kujisajili katika mtandao wa Tuzo hizo kwa barua pepe (email )zao kisha watachagua Bara la Afrika  na kisha kwenda kipengele cha kivutio bora cha Bara la Afrika na kupigia kura Ngorongoro.

No comments