HEADER AD

HEADER AD

RC KAGERA : UMASKINI CHANZO CHA HUSDA INAYOLETA MIGOGORO KWENYE JAMII


Na Alodia Babara, Bukoba

MKUU wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amesema umaskini chanzo kikubwa kinachosababisha husda ambayo huleta migogoro katika jamii  na kisha kuzaa Taifa lisilo na maadili ya kimungu na kuleta uvunjifu wa amani. 

Ametoa kauli hiyo jana jioni wakati wa futali maalum iliyoandaliwa na mkuu huyo wa mkoa na kushirikisha watu wa kada mbalimbali wa kutoka Wilaya zote za mkoa huo.

     Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa akizungumza katika futari maalum iliyoandaliwa na ofisi yake

"Viongozi wetu Mashekhe katika hotuba zao pamoja na kuzungumzia masuala ya zaka, Ramadhani pia wamezungumzia umoja na mshikamano na kutuasa tusiwe na husda ambayo kwa kiasi kikubwa huchochewa na umasikini wale ambao hawana wanawaona wenzao roho inawauma na badala ya kuuliza alipataje au kutumia fulsa akusaidie nawewe kupata unaanza kumpiga vita na kupambana naye"

Amesema hari hiyo maarufu kwa lugha ya Kagera inaitwa kamunobele inapaswa kupigwa vita na kila mtu, pia kuna dhamira ya dhati ya kutorohusu mtu yoyote kutumia njia yoyote kuchonganisha Kagera bali watashikamana kusaidiana katika shida na raha.

Amesema kufungamana katika kujiletea maendeleo bila kujali imani za itikadi za dini zao, makabila,tofauti zao za kisiasa na mengine mengi wawe timu moja wanaijenga Kagera.


"Tutumie fursa zinazoletwa na Serikali tuwahimize watoto na familia zetu kutumia ardhi tuliyonayo kuzalisha na kujiletea maendeleo kwasababu wapo wageni tuliowakaribisha zamani kama vibarua leo wanatugharimu kwa kudai wao ni raia wa nchi hii hususani mkoa huu.i

" Ipo siku wanaweza kujimilikisha ardhi yetu na sisi kujikuta tunabaki tukihangaika na vizazi vyetu vikikosa fursa hii.

Wakati huo huo, Ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kutoa fedha nyingi ya kutekeleza miradi mbalimbali  ya maendeleo ambapo maonbi ya mkoa wa Kagera yameingizwa kwenye bajeti ya Serikali.

Kwa upande wake shekhe wa mkoa wa Kagera Haluna Kichwabuta amewataka waumini wa dini ya kiislam kudumisha amani na utulivu muda wote iwe wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwani hiyo ni Neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

          Wananchi wakishiriki futari 

"Tumeweza kukaa hapa na kufuturu kwa kujiamini kutokana na amani iliyopo hapa nchini hivyo kuanzisha kinyume cha amani na utulivu ni kukufuru Neema ya mwenyezi Mungu ambayo inaweza kusababisha watu kupata adhabu ikiwemo vita, njaa na kukimbia huku na kule"amesema Kichwabuta.

Amesema kuwa yeye anamfananisha Rais Samia kama mti mzuri unaotoa matunda kutokana na mambo makubwa ambayo anayafanya na kuendelea kuyatekeleza ikiwemo ujenzi wa madaraja makubwa, Leli, kuongeza ndege mpya na mengine mengi.

Naye Shekhe Abdulshahidu Abbas Amiri kutoka Taasisi ya Kiislam kanda ya ziwa (JASUTA) amewaasa waislamu kuachana na migogoro, mizozo kwa  sababu hurudisha maendeleo nyuma.

Amesema watu hudhoofika wale wanaoishi na mizozo ndani yake iwe familia chama cha siasa basi fanyeni haraka kuondoa hari hiyo kwasababu hiyo ni raana, inapelekea Taifa kuwa dhaifu.

     Shekhe Abdushahidu Abbas Amiri kutoka taasisi ya kiislamu (JOSUTA) kanda ya ziwa akizumgumza wakati wa futari iliyotolewa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera.

No comments