HEADER AD

HEADER AD

SERIKALI KUTANGAZA MATOKEO SENSA YA WANYAMAPORI, RIPOTI YA WATALII WALIOTEMBELEA TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Arusha

SERIKALI ya Tanzania kupitia wizara ya Maliasili na Utalii inatarajia kutangaza rasmi matokeo ya sensa ya wanyamapori pamoja na kuzindua ripoti ya Watalii wa Kimataifa walioitembelea nchini kwa mwaka 2023.

Utangazaji  na uzinduzi huu utafanyika Aprili, 22, 2024, utajumuisha wadau mbalimbali wa uhifadhi na utalii utafanyika katika Hoteli ya Gran Melia  Jijini Arusha ambapo Waziri wa maliasili na utalii Angellah Kairuki ndiye anayetarajiwa kutangaza matokeo hayo ya sensa na kuzindua ripoti hiyo.

Katika mkutano wake na wanahabari  jijini Arusha, Mwakilishi wa Wizara ya Maliasili  na  Utalii  Dkt. Edward  Kohi  ambaye ni Mkurugenzi  wa Utafiti  na Mafunzo  amesema taarifa hizo zenye  tija katika uhifadhi wa wanyamapori na kukuza utalii nchini zinaakisi juhudi za Serekali  kuhifadhi  utajiri  wa Maliasili ya Wanyamapori na kukuza utalii nchini.

       Mkurugenzi  wa Utafiti  na Mafunzo Dkt. Edward Kohi

Aidha ripoti hiyo itaangazia matokeo ya watalii walioitembelea Tanzania mwaka 2023 baada ya Rais  Samia Suluhu  Hassan kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia filamu ya Royal  Tour



No comments