HEADER AD

HEADER AD

VYUO VIKUU VYASHIRIKI MASHINDANO YA LUGHA YA KICHINA DAR

Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam 

VYUO vikuu vinne ikiwemo Chuo Kikuu cha Mlimani (UDSM), Chuo kikuu Kishiriki cha Mkwawa (MUCE), Chuo kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) na Mwalimu Nyerere vimeshiriki Mashindano ya 23 ya Lugha ya Kichina ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania ya kuimba na kuzungumza, yaliofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). 

Awali katika shindano hilo, Profesa Rutinwa amesema wanafunzi wa kitanzania wamekuwa na mwamko wa kusoma lugha ya kichina kila mwaka hadi kufikia 1000 katika program tofauti kupitiaTaasisi ya Kichina ya Confucius iliyoko UDSM.

Amesema taasisi hiyo ni muhimu katika kubadilishana utamaduni na ujifunzaji wa lugha ya kichina kama mbinu madhubuti ya kukuza na kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

        Wanafunzi wa vyuo vikuu wakifuatilia mashindano

Kwa upande wake Mkurugenzi Mwenza wa taasisi hiyo ya kichina hapa nchini, Profesa Aldin Mutembei amesema anafurahia kuona umahiri wa wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali katika lugha na utamaduni wa kichina.

“Ninajua bila shaka mmejiandaa vya kutosha. Ni vizuri kutuonesha mlivyojiandaa lakini kumbuka tungependa washindi watakapopatikana wafanye vizuri zaidi huko watakakokwenda.

“Mashindano haya huenda hatua kwa hatua hadi kushindanisha washindi katika nchi, katika kanda, katika bara na baadaye katika dunia.

Tungependa nanyi mtakaposhinda mtuwakilishe huko duniani,” amesema.

Katika shindano hilo, Mwanafunzi Aman Njohole kutoka DUCE ameonesha shauku yake ya kuwa kinara ilikutimiza ndoto zake.

Aman Njohole kutoka Chuo kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) 

"Natamani kuwa kinara katika mashindano haya ya kujifunza lugha ya kichina, niweze kuitangaza Tanzania kwa kuonyesha kuwa lugha hii, mtu  yeyote anaweza kujifunza,”. Amesema Njohole .

Njohole ameongeza kusema kuwa ameshiriki shindano hilo kwani ndoto yake ni kuwa mwalimu wa lugha ya kichina.

Naye Mwalimu kutoka MUCE, Tawi la Confucius Dar es Salaam, Shariff Matumbi amesema machindano hayo yamekuwa yakiongezea wanafunzi uwezo wa kujua lugha hiyo kwa wepesi kupitia nyimbo, kuzungumza na mambo mbalimbali kwa kuwa hivi sasa lugha hiyo imekuwa na soko kubwa hapa nchini na hata ulimwenguni.



No comments