HEADER AD

HEADER AD

FCC, TRADEMARK AFRIKA WASAINI MKATABA WA KULINDA MLAJI NA KUDHIBITI BIASHARA BANDIA


Na Andrew Charle, Dar es Salaam

TUME ya Ushindani (FCC) na TradeMark Africa (TMA) wamesaini mkataba wamashirikiano wa miaka mitatu katika kuunga mkono utekelezaji wa shughuli za tume hiyo yaani (Partner Support Agreement -PSA)  katika kulinda na kushaghisha ushindani katika kulinda mlaji na kudhibiti biashara bandia.

Tukio hilo la mkataba wa awali umegharimu kiasi cha Tsh. 1.56 Bilioni, limefanyika Mei, 27, 2024 Dar es Salaam ambapo limeshuhudiwa na watendaji wa pande zote mbili mbele ya Waandishi wa Habari.

       Mkurugenzi Mkuu wa FCC William Erio, (wa pili kulia), na Mkurugenzi wa Trademark Africa, Elibariki Shammy, (kushoto) wakisaini mkataba wa mashirikiano kati ya Taasisi hizo

Awali Mtendaji Mkuu wa FCC, William Erio amesema kuwa TMA wamekuwa wakifanya mambo mengi ikiwemo kuhakikisha shughuli za ukuaji wa kibiashara na Tanzania inakuwa na sehemu nzuri ya uwekezaji.

Mtendaji mkuu huyo William Erio ameeleza kuwa katika mkataba huo, TMA watahakikisha shughuli za utendaji za FCC zote zinakwenda Kidijitali, Kuboresha kwa kiwango kikubwa miundombinu ya Tehama na taasisi, na mwisho kuwa na mafunzo kwa wafanyakazi katika kuhakikisha wanafanya kazi vizuri na kwa haraka zaidi na kwa ufanisi unaotarajiwa na wawekezaji.

  Mkurugenzi Mkuu wa FCC William Erio, (kulia), na Mkurugenzi wa Trademark Africa, Elibariki Shammy, (kushoto) wakionesha hati za mikataba baada ya kusaini Jijini Dar es Salaam.

“Matokeo yake ni kwamba muda wa kushughulikia maombi mbalimbali ya kibiashara utapungua sana na gharama za utekelezaji pia zitakuwa ndogo.

Na tunaamini pia hii itaendana sambamba na muelekeo wa awamu ya sita chini ya Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye amekuwa anasafiri katika nchi mbalimbali akipigania nchi yetu ipate maendeleo ya kiuchumi kwa kuvutia wawekezaji na wafanyabiara kuja kuwekeza na kufanya biashara ndani ya nchi yetu.

" Lakini pia kuiwezesha nchi yetu kunufaika na fursa za kufanya biasara katika masoko mbalimbali ikiwemo AfCFTA, Jumuiaya ya Afrika Mashariki, Jumuiya za kiuchumi Kusini mwa Afrika (SADC),  na zingine nyingine.’’ Amesema Bw. William Erio.

Amesema mkataba huo ni katika kuhakikisha wanaelekea katika Tanzania ambayo Rais anaikusudia ifikiwe, itafikiwa na maendeleo kwa ujumla wake yatapatikana.

Mkurugenzi Mkuu wa FCC William Erio, akizungumza na waandishi wa Habari muda mfupi baada ya kumalizika zoezi la kusaini makubaliano hayo

Mkurugenzi Mkuu wa FCC William Erio, akizungumza na waandishi wa Habari muda mfupi baada ya kumalizika zoezi la kusaini makubaliano hayo.

Mkurugenzi Mkaazi wa Trademark Africa, Bw Elibariki Shammy ameshukuru Serikali ya Tanzania pamoja na FCC kwa kile anachoamini mkataba huo unaenda kujenga utendaji kazi bora huku akisisitiza kuwa ni muhimu kwa malengo ya kimkakati ya kuchochea ukuaji wa biashara ambao ni endelevu na shirikishi.

Mkurugenzi wa Trademark Africa, Elibariki Shammy, (kushoto) akiongea na waandishi wa Habari katika hafla hiyo

Trademark Africa inatekeleza mradi huo ambao umefadhiliwa na Serikali ya Uingereza, Jumuia ya Madola, Ireland na Norway.

No comments