HEADER AD

HEADER AD

WAZIRI MKUU AWATAKA WAKAZI WA GEITA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UVUVI


Na Daniel Limbe, Chato

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa, amewataka wakazi wa mkoa wa Geita kujikita kwenye sekta ya uvuvi ili kuongeza ajira na kuinua vipato vyao.

Aidha amesema serikali ya awamu ya sita imejikita kusogeza karibu miradi ya maendeleo ili kuwapa fursa za kiuchumi wananchi wake huku akiwasisitizia kufanya kazi kwa bidii.

Ameyasema hayo akiwa kwenye uwekaji wa jiwe la msingi wa mradi mkubwa wa kisasa wa soko la samaki lilipo wilayani Chato mkoani humo.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa  (wa kwanza kushoto) akizungumza.

Hata hivyo amesema kukamilika kwa ujenzi wa soko hilo utasaidia kuinua uchumi wa wananchi, wilaya na taifa kwa ujumla na kwamba wafanyabishara kutoka nchi za Kongo na Burundi wanatarajiwa kutumia soko hilo kununua mazao ya samaki.

Ameongeza kuwa, hatua hiyo itaimarisha mahusiano ya nchi wanachama wa Afrika mashariki lengo likiwa ni kuinua uchumi wa wananchi na kupunguza umaskini wa vipato.

           Samaki wakiuzwa

Awali msimamizi mkuu wa mradi wa ujenzi wa soko hilo,mhandisi George Kwandu, akizungumza kwa niaba ya Katibu mkuu wa wizara ya Mifugo na Uvuvi,amesema miradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 1.7 unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti 2024.

             Soko la kisasa la Samaki

" Soko hilo litahusisha ufungaji wa mitambo ya kukausha samaki na jengo la uzalishaji barafu ambayo pia itauzwa kwa wavuvi wengine wanaojihusisha na uongezaji thamani ya mazao vya uvuvi" amesema.

Ameongeza kuwa soko hilo litakuwa na uwezo wa kukausha tani 10 za samaki aina ya dagaa na samaki wengine kuhifadhiwa kwa zaidi ya saa 240 pasipo kuharibika.

                    

No comments