VIJANA WA KISABATO MTAA WA MATONGO –NYAMONGO WAFUNGUA MAKAMBI KWA MAANDAMANO
Na Dinna Maningo, Nyamongo
KANISA la Waadventista Wasabato Mtaa kivuli wa Matongo- Nyamongo wilayani Tarime, Mkoani Mara wamefungua sikukuu ya vibanda maarufu Makambi.
Vijana wamefanya maandamano kwa kutembea wakipita maeneo mbalimbali kama njia ya kuwakaribisha waumini na wananchi kwa ujumla kushiriki makambi.
Vijana wa Kisabato mtaa wa Matongo wakiwa kwenye maandamano wakati wa ufunguzi wa makambi katika mtaa kivuli wa Matongo- Nyamongo.Makambi yamefunguliwa rasmi na Mchungaji Samweli Kihine ambayeni ni mchungaji wa mtaa huo unaobeba makanisa matatu ambayo ni Matongo, Kwimange , Kegonga pamoja na kundi la Nyabibago.
Kanisa la Waadventista Wasabato Matongo
Makambi hayo ni ya nne katika mtaa huo kivuli yenye kauli mbiu isemayo ; Makambi 2024 : Nitakwenda na Familia yangu.
Benjamin Musa kiongozi wa Vijana mtaa wa Matongo, ameiambia DIMA Online kuwa vijana wakiwemo Watafuta njia, Wavumbuzi ambapo wanawakaribisha watu wote kushiriki makambi yanayofanyika maeneo ya Byasuma katika kanisa la Matongo.
Benjamin Musa kiongozi wa Vijana mtaa wa Matongo’’Tumefungua Mkambi leo, na sisi kama vijana tumeweza kutembea kuanzia kanisa la Kwimange tukafika hadi kanisa la Kengonga tukaendelea na safari hadi Kitongoji cha Kwinyunyi kisha Kanisani Matongo.
Ameongeza kusema ‘’ Tunawakaribisha watu wote kushiriki katika makambi yetu. Kila tulikopita tumewajulisha wananchi kwa kuwatangazia kupitia vipaza sauti ili washiriki nasi kwenye makambi.
" Tunawakaribisha sana kutakuwa na mafundisho mbalimbali na maombi kupitia wachungaji na viongozi mbalimbali wa kanisa, vijana wataonesha programu zao, kwaya zitaimba hakika siyo ya kukosa ‘’ amesema Benjamini.
Mchungaji Samwel amefungua mafunzo hayo ambapo amesema lengo la kuhudhulia makambi ni pamoja na kumshukuru Mungu kwa kuwavusha mwaka mzima salama, Maungamo na Toba.
Vijana wa Kisabato kanisa la Kwimange wakiimba
Post a Comment