HEADER AD

HEADER AD

WATANZANIA WAOMBWA KUMSAIDIA ALLY KARUME




Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

NAIBU Meya wa Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Michael Urio amewaomba watanzania wakiwemo viongozi wa serikali kumsaidia matibabu na huduma mbalimbali Ally Karume Ally mwenye umri wa miaka (41) mkazi wa Kilungule Mbagala, Wilaya ya Temeke.

Mgonjwa huyo yupo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wodi namba 11, akipatiwa matibabu.

      Naibu Meya wa manispaa ya Kinondoni Michael Urio akizungumza na Ally Karume Ally.

Naibu Meya ambaye amefika katika hospitali hiyo Agasti, 27, 2024 kumjulia hali mgonjwa huyo anayesimamiwa kwa ukaribu na Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Dar es Salaam (DCPC).

Akizungumza na Waandishi wa habari Urio amesema Kalume yupo kwenye maumivu makali na kuuomba uongozi wa hospitali kumsadia kwa hali na mali.

   Naibu Meya wa manispaa ya Kinondoni Michael Urio pamoja na Mkurugenzi wa Upasuaji katika hospital ya Taifa ya Muhimbili Dk. Rachel Mhavile , wakimjulia hali Ally Karume Ally .

"Nimefika wodini, nimebahatika kumuona ndugu yetu, kwa kweli yupo kwenye maumivu makali sana, ameniambia na nimemuona.

"Ombi langu kwa uongozi wa hospitali ya Muhimbili tumsaidie ndugu yetu huku sisi tukiendelea kuiomba jamiii imsaidie kwa hali na mali, naamini tutafanikiwa.  Mawaziri, Wabunge, Madiwani na watu mbalimbali naomba wamsaidie kwa chochote" ameomba Urio .

Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi wa huduma za upasuaji Dk. Rachel Mhavile amesema, mgonjwa huyo alipokelewa Agost 24 akitokea Hospitali ya Temeke na tayari ameshafanyiwa vipimo vyote. 

"Tayari ameshachukuliwa vipimo vyote na tunangoja vipimo tuone tunaanzia wapi, kwa sasa anapewa dawa za kutuliza maumivu , " amesema Dkt. Mhavile.

Nae Mwakilishi wa kamati ya kuratibu matibabu ya mgonjwa huyo kutoka DCPC, Careen Mgonja, ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili kuwa karibu na mgonjwa huyo katika kumpatia matibau huku akiomba wadau na watu mbalimbali kuendelea kuchangia kupitia namba maalum ya aliyeteuliwa.

     Mwakilishi wa kamati ya kuratibu matibabu ya mgonjwa huyo kutoka DCPC, Careen Mgonja

" Watu wote watakaoguswa kusaidia kuchangia mgonjwa wanaweza kutuma kiasi chochote cha pesa kupitia kwa Mratibu Mkuu wa zoezi hili, Bi. Kalunde Saidi kupitia namba ya Mtandao wa Airtel 0684695698 Jina Kalunde Saidi.

Naibu Meya wa manispaa ya Kinondoni Michael Urio pamoja na Mkurugenzi wa Upasuaji katika hospital ya Taifa ya Muhimbili Dk. Rachel Mhavile , wakiwa katika huzuni baada ya kumuona  Ally Karume Ally.




No comments