HEADER AD

HEADER AD

MWENYEKITI WA CCM BARIADI AFARIKI DUNIA

 

Na Samwel Mwanga,Simiyu

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu,Juliana Mahongo amefariki dunia Septemba 15 akiwa nyumbani kwake mtaa wa Somanda mjini Bariadi majira ya saa 1:00 asubuhi.

Katibu wa CCM wilaya ya Bariadi, Ibrahim Kijanga ameiambia DIMA ONLINE kwa njia ya simu kuwa Mwenyekiti huyo mara baada ya kufikwa na mauti hayo mwili wake ulipelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo iliyoko eneo la Nyaumata mjini Bariadi.

Mwenyekiti huyo hadi amekutwa na mauti amekuwa akihudumu katika nafasi hiyo kwa vipindi  vinne mfululizo.

Amesema kuwa taarifa ya chanzo cha kifo hicho itatolewa na familia sambamba na mipango ya mazishi inaandaliwa na familia na itakapokamilika CCM wilaya ya Bariadi itajulishwa na kutoa taarifa kwa wananchi.

Katibu huyo amemtaja Marehemu  Mahongo kama kiongozi ambaye alikuwa mtiifu, mwaminifu na mzalendo kwa chama chake.

No comments