HEADER AD

HEADER AD

NYAMBARI NYANGWINE : VIJANA WASIKIMBILIE KUAJIRIWA WAJIAJIRI

>>Asema waliofanikiwa wengi Duniani ni waliojiajiri


>>Askofu Msongazila aomba makundi ya hali ya chini yawezeshwe

Na Dinna Maningo, Tarime
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Nyambari Nyangwine na aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Tarime, amewaomba vijana nchini kijiajiri badala ya kutegemea kazi za kuajiriwa.

Nyangwine ameyasema hayo Septemba, 29, 2024 wakati wa harambee  ya ujenzi wa Kanisa Parokia ya Mtakatifu Mathayo Mwinjili lililopo Kijiji cha Kesangora katika Kata ya Nyamwaga, Jimbo Katoriki la Musoma.

       Nyambari Nyangwine aliyevaa kofia akizungumza na viongozi.

Amesema kuwa Duniani watu waliofanya maendeleo na kufika mbali wengi wao sio waajiriwa bali wamejiajiri hivyo ni vyema vijana wakajiajiri katika shughuli mbalimbali za ujasiliamali.

" Vijana wasikimbilie kuajiriwa Wajiajiri . Ujasiriamali ni suala la msingi sana. Katika elimu ya Tanzania mitaala imeboreshwa somo la maadili na ujasiliamali limeingizwa shuleni na linatumika, kwahiyo wanafunzi wetu someni sana.

" Dunia nzima watu waliofanya maendeleo na wakafika mbali wengi wao sio waajiriwa wamejiajiri  nawaombeni fanyeni ujasiriamali " amesema Nyambari.

Pia amesisitiza suala la maadili kwani linasaidia watu kusonga mbele huku akiwahimiza wazazi kukomesha watoto kwakuwa elimu ni suala la msingi sana.

           Nyambari Nyangwine akipokelewa kwa shangwe baada ya kuwasili kanisani kwa ajili ya kuchangia fedha za ujenzi wa kanisa

Askofu wa Jimbo Katoriki Musoma Michael Msongazila ameomba makundi ya hali ya chini yawezeshwe yapande yaweze kutoa huduma vizuri kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, jamii na kwa ajili ya sifa na utukufu kwa mwenyezi Mungu.

" Wapo vijana wengi wanamaliza kidato cha nne na cha sita kwenda chuo kikuu ni shida , na hata wakienda chuo kikuu wakimaliza bado ajira ni shida.

       Askofu wa Jimbo Katoriki Musoma Michael Msongazila akizungumza wakati wa harambee ya ujenzi wa Kanisa.

" Tunapopata makundi ya watu wanaoweza kuoana mbali na kuleta maendeleo basi hayo makundi yaliyobaki bila ajira yanaweza kueleweshwa vizuri na yakafanya kazi vizuri. Sisi tulio na nafasi tutumie nafasi hiyo kuyaendeleza makundi madogo.

Ameongeza " Nimshukuru Nyambari Nyangwine kwa kuanzisha shirika linalojihusisha na masuala ya kijamii, naamini inajibu maswali haya ya kutetea haki na amani, ustawi wa makundi yasiyoangaliwa vizuri.

" Tutumie nafasi ya hawa watu watusaidie katika kumwendeleza binadamu bila kusahau amani ya ndani na maendeleo ya kweli " amesema Askofu Msongazila.





No comments