HEADER AD

HEADER AD

VIONGOZI CHADEMA WALIOKAMATWA WAACHIWA

VIONGOZI wakuu wa chama cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) nchini Tanzania waliokamatwa kwa kutaka kufanya maandamano wameachiwa.

Chama hicho kimesema, baada ya kushikiliwa na polisi ambao walizuia maandamano yaliyokuwa yamepangwa jijini Dar Es Salaam katika hatua ya hivi karibuni ni kuwanyamanzisha wapinzani.

Licha ya marufuku iliyotolewa CHADEMA kiliapa kusonga mbele na maandamano ya kupinga kile kinachodaiwa ni kulaani utekaji nyara na mauaji ya wanachama wake yanayofanywa na maafisa wa Polisi.

Polisi wa kuzima ghasia walikuwa wamejipanga jijini kote wakiwa na mabomu ya kurusha maji ya kuwasha ili kuzuia mikusanyiko, na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Makamu wake Tundu Lissu walikamatwa haraka pamoja na wengine kadhaa.

Baadaye Jumatatu jioni, chama hicho kiliandika kwenye mtandao wa X kwamba Mbowe na Lissu, pamoja na afisa mwingine mkuu wa chama, waliachiliwa kwa dhamana.

Hata hivyo, Mbowe “aliamua kubaki katika kituo cha polisi hadi wanachama na wafuasi wengine waliokamatwa wapewe dhamana,” Chadema kimesema.


No comments