HEADER AD

HEADER AD

WORLD VISION TANZANIA YATUMIA BILIONI 10 KUTEKELEZA MIRADI SIMIYU

Na Samwel Mwanga, Itilima

SHIRIKA la World Vision Tanzania kupitia wafadhili kutoka Marekani limetumia zaidi ya Tsh. Bilioni 10.4  kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za mradi katika kuboresha sekta za Elimu, Afya na lishe, Maji, Kilimo na Mifugo,Uchumi wa Kaya,Usafi wa mazingira.


Pia kuongeza uchumi wa kaya pamoja na usalama na ulinzi wa mtoto katika kata sita za Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.

 

Akitoa taarifa ya kufunga Mradi wa Maendeleo ya jamii Kanadi (Kanadi AP) ulioanza mwaka 2002, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la World vision Tanzania, James Anditi amesema pamoja na kumalizika kwa ufadhili wa shughuli katika kata za Bumela, Migato ,Mhunze, Ikindilo, Chinamilina Ndolelezi bado wanaendelea kutekeleza miradi mingine katika mkoa huo.


    Mkurugenzi Mkuu, Shirika la World Vision Tanzania,James Anditi akizungumza wakati wa sherehe za kufunga Mradi wa Kanadi AP kwenye viwanja vya Nanga Shule ya Msingi wilayani Itilima

Amesema kuwa katika kipindi cha miaka 22 ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali Mradi huo wa Kanadi AP umeweza kuwafikia na kuwanufaisha jumla ya kaya 8005 zenye jumla ya watu 43,967 wakiwemo watu wazima na watoto.

“Naishukuru Serikali ya Tanzania kwa kukubali sisi pamoja na wafadhili wetu wa Marekani kuwa ni sehemu ya kuchochea maendeleo kwa wananchi wetu  hapa nchini.


" Natumaini kwa miaka hii 22 tuliyokaa hapa Kanadi tumefanya kazi kwa weledi mkubwa ndio maana  tumeleta mabadiliko makubwa kwenye sekta zote tumezigusa kwa karibu sana, mimi nawatakia kila la kheri wananchi wa Kanadi na kata zote tulipokuwa tukitekeleza mradi hiyo,” amesema.


 

      Mkurugenzi Mkuu,Shirika la World Vision Tanzania,James Anditi (aliyekati) akipokea zawadi ya boksi la sabuni zilizotengenezwa na kikundi cha wanawake waliowezeshwa na shirika hilo kupitia Mradi wa Kanadi AP.

Ameongeza “Kwa jamii ya Kanadi ninapenda kuwashukuru sana kwa kukubali kutoa ushirikiano wenu kwetu kwa kushiriki katika shughuli za ufadhili wa watoto, kufuatilia na kushiriki kikamilifu kwenye shughuli zote za utekelezaji wa miradi mbalimbali.


"Tunawashukuru kwa kujitoa kwa hali na mali katika kuchangia shughuli za maendeleo katika eneo lenu hakika mchango wenu ulikuwa wa thamani kubwa na hii ni ishara njema kuwa hata bila ufadhili wa nje Jamii ya Kanadi itaendelea kusonga mbele katika kujiletea maendeleo endelevu,”amesema.

 

Pia ametumia nafasi hiyo kutoa ombi kwa uongozi wa serikali katika mkoa huo kuwa mafanikio yaliyopatikana kupitia Mradi huo ni vizuri yakaendelea kusimamiwa vyema na kudumishwa ili kuenzi moyo na upendo kutoka kwa wafadhili wa Marekani na kudumisha ustawi wa watoto katika kaya na jamii ya Kanadi ya leo na kwa kizazi kijacho.


       Mkurugenzi Mkuu,Shirika la World Vision Tanzania,James Anditi (aliyekati) akipokea zawadi ya Asali kutoka vikundi vya walina asali waliowezeshwa na shirika hilo kupitia Mradi wa Kanadi AP

 

Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Mradi wa Kanadi Ap, Dotto Mgema amesema kuwa Shirika hilo kwa kipindi cha miaka 22 lilichofanya kazi kwenye eneo la mradi huo likeweza limebadilisha maisha ya wananchi wa eneo.


Ametolea mfano katika Kilimo na Usalama wa Chakula ambapo wakulima walijengewa uwezo kwa kupewa mafunzo ya kilimo bora ambapo kwa sasa utumiaji wa pembejeo bora umeongezeka na uzalishaji kwa ekari kutoka gunia 6 ya kilo 100 za mahindi hadi gunia 15.


       Baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati wa sherehe za kufunga mradi wa Kanadi AP katika viwanja vya shule ya Msingi Nanga wilayani Itilima mkoa wa Simiyu.

Amesema kuwa zaidi ya ng’ombe 500 wa maziwa, Mbuzi 100 wa maziwa, Mizinga 500 kwa wafugaji wa nyuki, ukarabati wa majoyysho mawili kwa ajili ya kuogeshea mifugo na kuanzishwa kwa vikundi vya hisa zaidi ya 213 vya kuweka na kukopa vimeweza kuunganishwa kupata mkopo kutoka Shirika la la Vision Fund ambapo zaidi ta Sh

236,600,500/= zimetolewa kama mkopo ikiwa ni sehemu ya miradi iliyotekelezwa.

 

Amesema kuwa miradi mingi ya maji vikiwemo visima vifupi na virefu vimechimbwa na maji kusambazwa kwenye jamii zikiwemo taasisi za serikali kama vile shule na zahanati katika kijiji cha Nangale ambapo kuna mradi mkubwa wa maji ya bomba. 


    Naibu Waziri wa maji,Mhandisi Kundo Mathew(kushoto)akikagua kituo cha kuchotea maji katika kijiji cha Nangale uliotekelezwa na Shirika la World Vission Kanadi.


Pia wameweza kuhakikisha wanatoa mchango mkubwa katika sekta ya elimu kwa kujenga madarasa shuleni na kuhakikisha watoto wanajua kusoma, kuhesabu na kuandika kwa viwango vinavyokubalika ili kuhakikisha ya kuwa watoto hao wanapomaliza elimu ya msingi ili waweze kujitegemea kuwa na stadi mbalimbali wamejenga Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Kanadi(Kanadi VTC).

 

Katika kuhakikisha suala la ulinzi na usalama wa mtoto, shirika hilo kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Itilima wametoa mafunzo juu ya haki za mtoto na ushirikishwaji na matokeo yake kwa sasa watoto wa kike na kiume wanashiriki katika elimu katika usawa.

 

Mbunge wa Jimbo la Itilima, Njalu Silanga amelipongeza shirika hilo katika kutekeleza miradi huku akiomba kama kuna uwezekano wa kutekeleza mradi mwingine katika wilaya hiyo watekeleze kwani wao ni wadau muhimu katika kusaidiana na serikali kuchochea maendeleo hapa nchini.


“Mie Mbunge wa Jimbo la Itilima nikiri mbele yenu ya kuwa wananchi wa Kanadi wamenufaika na mradi huu katika kuleta mabadiliko makubwa hasa katika maeneo ya sekta ya Elimu , Afya, Mazingira na Maji.


" Tunawashukuru kwa kujitoa, tunaahidi kuyaendeleza yote yaliyo mema na kutumia ujuzi mlio upandikiza kwetu kwa muda wote wa miaka 22,”amesema.

 

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Sherehe hizo za kufunga mradi huo ameseka kuwa serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetengeneza mazingira mazuri ya Diplomasia ya Kimataifa kwa mataifa mbalimbali kuja kuwekeza nchini na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama walivyofanya Shirika la World Vision Tanzania.


         Naibu Waziri wa Maji,Kundo Mathew akizungumza wakati wa sherehe za kufunga Mradi wa Kanadi AP kwenye viwanja vya Nanga Shule ya Msingi wilayani Itilima

Amewataka wananchi wa Kanadi na wilaya ya Itilima kwa ujumla kutosikitika Shirika la World Vision kuondoka kwa kuwa tayari limewajengea uwezo wa kujitegemea kupitia Serikali. Tunawashukuru sana kwakuwa nanyi kwenye kusukuma maendeleo ya wana Simiyu na watanzania pia. 

 

“Hatupaswi kunung’unika, kikubwa  tunatakiwa kuwashukuru sana World Vision kwa miaka yote 22 kuwa na sisi. Tuvitunze, kuvilinda na kuvithamini hasa kwa umakini mkubwa sana na kutumia maarifa tuliyo achiwa na wadau wetu wa maendeleo kuviendeleza zaidi maana kama maarifa wametuachia ya kutosha,”amesema.


No comments