HEADER AD

HEADER AD

MAIN FM, POLISI, HOSPITALI YAANDAA MASHINDANO YA MPIRA KWA WAENDESHA PIKIPIKI KIGOMA

>> Lengo ni kuhamasisha usalama barabarani, afya ya uzazi


>>Bodaboda Mlole yaichapa mabao 5-1 Bodaboda Bangwe

>>Kampuni ya gesi ya kupikia ya Oryx kutoa mitungi kwa timu zitakazoshinda

Na Editha Karlo, Kigoma
 
TIMU nane za waendesha pikipiki (Bodaboda) zimeanza kupambana katika ligi maalum kwa ajili ya kuhamasisha masuala ya usalama barabarani na masuala ya afya ya uzazi huku Mshindi wa mashindano hayo akitarajia kuibuka na kitita cha Tsh. Milioni moja.

Mkurugenzi wa kituo cha Radio cha Main FM ambao ndiyo waandaaji wa mashindano hayo, Pascal Willian amesema kuwa mashindano hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Radio hiyo, jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani mkoa Kigoma na Hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma Maweni na kufafanua kuwa mashindano hayo pia yatatumika kuhamasisha masuala ya uwekezaji.

          Pascal Willian Mkurugenzi wa Main FM akizungumza na waandishi baada ya mechi ya ufunguzi

Mashindano kipenga cha mashindano hayo kimepulizwa na Mkuu wa wilaya Kigoma, Dk. Rashid Chuachua aliyemwakilishwa na Afisa Tawala wa wilaya Kigoma Dola Buzaire.

Dola amesema kuwa mashindano hayo yana maana kubwa katika kuhimiza usalama barabarani lakini pia kuhimiza suala la watu kufanya mazoezi na kushiriki michezo.

         Dolla Buzaire Afisa Tawala wa wilaya Kigoma aliyemwakikisha Mkuu wa wilaya Kigoma Dk.Chuachua
 
Katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo yanayofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Kawawa Ujiji mjini Kigoma timu ya kombaini ya Bodaboda Mlole imeifunga Kombaini ya bodaboda ya Bangwe kwa jumla ya Magoli 5 – 1.
 
Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo Mwakilishi wa kampuni ya gesi ya kupikia ya Oryx, Gibson Rodgers amesema kuwa kampuni hiyo itakuwa ikitoa mtungi mdogo wa gesi kwa kila mchezo kwa mchezo bora wa mechi ikiwa ni sehemu ya udhamini wao wa mshindano hayo kuchochea vijaana kujituma Zaidi uwanjani.

       Washindi katika mechi ya ufunguzi kombaini ya Bodaboda Mlole (jezi nyeupe) na Kombaini ya bodaboda Bangwe jezi za bluu


     Mwakilishi wa kampuni ya gesi ya kupikia ya Oryx, Gibson  Rodgers (kulia) akikabidhi mtungi wa gesi kwa mchezaji wa kombaini ya Bodaboda Mlole ambaye alikuwa mchezaji bora wa mechi ya ufunguzi
 

No comments