HEADER AD

HEADER AD

MZAZI ALIVYODAIWA NG'OMBE SITA BAADA YA BINTI YAKE KUTOPATA MTOTO


 >> Ni miaka minane tangu aolewe hajafanikiwa kupata mtoto

>>Binti asimulia alivyoteswa 

>>Mahakama iliamuru mme arudishe mahali kwakuwa mkewe hajapata mtoto

Na Suzy Butondo, Shinyanga

Mkazi wa kijiji cha Bugomba B Kitongoji cha Shilabela kata ya Ubagwe   Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga  Petro Sayi   amejikuta akilia baada ya kudaiwa  Ng’ombe  sita  zilizotolewa kwaajili ya Mahari  ya kuolewa binti yake  nakurudishwa nyumbani kwa kudaiwa hazai.

Akizungumzia mkasa huo baba huyo wa familia Sayi ameeleza mkasa huo  mbele ya waandishi wa habari  waliofika kwenye kijiji hicho, ambapo alikuwa amewakusanya baadhi ya wazee na majirani walioshuhudia utolewaji wa ng"ombe hizo tangu mwaka 2017 alipokuwa akiolewa  binti yake.

Sayi amesema binti yake aliolewa na kuishi na mume wake katika kata ya Nyankende  kwa muda wa miaka minne, ambapo alishangaa  mwaka jana  binti yake kudangaywa na mume wake kuwa wazazi  wako wanakuhitaji ndipo alipomleta  akiwa alivyo vaa bila mzigo wowote nakumfikisha nyumbani kumkabidhi nakueleza  ameamua kumleta kwao kwa  sababu  hazai tangu amemuoa.

“Siku hiyo nilikua  nikiendelea kufanya kazi hapa nyumba bila kuja hili wala lile nilishtukia nikaona pikipiki inakuja nyumbani kwangu nikapsema nimepata wageni kumbe ameletwa mwanangu kaachika kwa kosa la kutozaa"alieleza Sayi.

"Niliwapokea huku nikiwa na furaha kuwa wamekuja na mme wake kutusalimia, walinisalimia na mkwilima wangu alinsalimiabaada ya salamu akaniambia kuwa amemrudisha binti yangu kwa sababu hazai.

" Nilinyamaza kimya baadae nikamshukuru na kumwambia nashukuru kwa kuwa umemrudisha akiwa mzima aliondoka mme wake nikabaki na mwanangu"aliendelea kueleza Sayi.

 "Baada ya mwaka mmoja nililetewa  taarifa ya kuitwa Mahakama ya Mwanzo  Mpunze nakutolewa hukumu kuwa nirudishe Ng’ombe saba sababu mwanangu ametia hasara alikoolewa  hazai ndipo nikajiuliza kumbe nirudishe   kama nilikopeshwa sio zawadi yangu kama mzazi"amesema  Sayi.

Aeleza mkasa uliompata

Binti aliyeolewa Anastazia  Sayi (21) amesema  aliolewa tangu mwaka 2017 baada ya kuolewa alifikia ukweni kwa mama mkwe, ambapo alikuwa akifanya kazi mbalimbali zikiwemo za kilimo na kuchunga mifugo.

"Nilikaa mwaka mmoja kwa mama mkwe baadae tukajitegemea mimi na mme wangu, tukatoka hapo kwa mama mkwe,lakini mama mkwe aliendelea kunifuatilia kwa kunitukana kwamba mimi mwanamke gani sizai hivyo alikuwa akimtaka mtoto wake aniache aowe mke mwingine"ameeleza Annastazia.

"Kwa kweli niliteseka sana mimi nilteseka kwa kuchunga mifugo ya ukweni na kupika, mama mkwe wangu  alikuwa akinitesa na kunilazimisha nifanye kazi zote kwa sababu sina faida zozote,  na alikuwa akimlazimisha mtoto wake  asinipende atafute mwanamke  mwingine ili mimi anirudishe  nyumbani kwetu kwa sababu  sizai  na wazazi wangu warudishe ng’ombe walizotoa"ameendelea kueleza.

“Nikiwa kwangu na mme wangu mama mkwe alimuita mume wangu akamueleza kwamba turudi kuishi naye, mme wangu alikubali tukarudi nyumbani tena na ndipo mateso yakaendelea  na hapo mme wangu alimshawishi  aniache aoe mke mwingine ndipo alipata mwanamke mwingine senta yaani madukani alianza kulala huko na kuniacha mimi nyumbani nikilala peke yangu"ameeleza.

" Niliendelea kuvumilia hivyo hivyo huku mama mkwe akimwambia mme wangu kuwa asiwe anaenda kwa mwanamke huyo bila kula awe anakula kwanza ndo aende, baadae aliowa mwanamke mwenye watoto  watatu  ambao siyo  watoto wake.

" Niliendelea kuvumilia hivyo hivyo, walipoona sishituki ndipo mme wangu alikuja na pikipiki akaniambia twende nyumbani kwenu tukawasalimie nilipanda kwenye pikipiki hivyo hivyo nilivyokuwa nimevaa,"

Tulipofika nyumbani nikashangaa nakabidhiwa kwa baba nikamuuliza mme wangu kuwa imekuwaje tena uliniambia tunakuja kusalimia tu na kurudi  hakunijibu akaondoka na mpaka sasa nipo.

"Mme wangu alikuwa ananipenda na mimi nampenda ila mama mkwe ndio alikuwa hanipendi ananiambia mimi mugumba sizaagi sifai kuendelea kukaa hapo ” anasema  Sayi.

Shuhuda  ambaye ni jirani wa familia hiyo Faustine  Kayanda anasema baada ya miaka mitatu waliitwa kama wazee kupata taarifa kuwa binti karudishwa  nyumbani sababu  hazai na kitu kilichowashangaza  mzazi kuombwa arudishe ng’ombe  mila na  desturi  za kabila la wasukuma Mahari ni zawadi.

"Kwa kweli na sisi limetushangaza sana hili binti wamekaanae miaka mnne akiwafanyia kazi mbalimbali halafu wanamrudisha na kuanza kudai mahali zao tena hadi kufikishana mahakamani sisi tunajua ukipewa mahali ni kama zawadi tu lakini mama mkwe wa huyu binti anataka Ng"ombre saba arudishiwe "anaeleza Kayanda.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji  hicho Msafiri Hussein anasema kweli familia hiyo ilifika ofisini kupata ushauri wakati akiwa mwenyekiti baada ya   binti  kurudishwa  nyumbani  na ng’ombe ziliamriwa kurudishwa ila walishauriwa  familia ya Sayi irudishe ng’ombe wawili au Tsh. laki mbili,  lakini hawakuafikiana walishangaa kesi ikaenda mahakamani nakutolewa hukumu ng’ombe zote zirudishwe.

“Nitoe  ushauri wangu kwamba  jamii ipewe elimu mahari  iwe kama zawadi  iandikishwe  ili badaye isiwe mateso kwa mzazi  sababu  unapopewa ng’ombe hizo na baadaye kudaiwa  hufikirii binti katumikishwa usiku na mchanga  naye kapata hasara hakuna wa kumuoa tena”alisema  Hussein.

Mama mkwe  wa binti huyo Lusia  Lushinge anasema kweli amemrudisha binti huyo na kudai ng’ombe ambazo alimpa mwanaye atoe mahari sababu binti hakukaa nyumbani kwake muda mrefu alikuwa akirudi nyumbani kwao bila faida yoyote na  kijana wake hayupo  amesafiri kwenda mkoani Katavi.

No comments