HEADER AD

HEADER AD

WAFANYAKAZI WANNE WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI

 

Na Gustaphu Haule, Pwani 

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za mauaji ya Juma Said Mfaume (40) mfanyabiashara na mkazi wa Mbagala Mlandizi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini Mkoani Pwani.

Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Muhudhwari Msuya amesema kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 7 mwaka huu katika kitongoji hicho .

Msuya,amesema kuwa katika tukio hilo wafanyakazi wa kampuni ya mikopo ya Oya walifika nyumbani kwa marehemu kwa lengo la kudai fedha za marejesho ya mikopo ya Oya zilizokopwa na mke wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khadija Ramadhani.

Amesema kuwa baada ya watuhumiwa kufika nyumbani kwa Juma Mfaume aliwaeleza kuwa mkewe hayupo lakini watuhumiwa hao walilazimisha kuingia ndani kwa nguvu kwa kumshambulia Mfaume sehemu mbalimbali ya mwili wake.

Msuya amesema watuhumiwa wakati wanaotumia nguvu hizo walikuwa wanatumia fimbo kumshambulia na ndipo akaanguka chini na kupoteza fahamu.

Ameongeza kuwa kutokana na hali hiyo watuhumiwa walimbeba Juma Mfaumekwa kutumia gari lao ili wampeleke hospitali lakini alifariki akiwa anapatiwa matibabu katika kituo cha afya Mlandizi.

Msuya amesema kutokana na kifo hicho mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na daktari na kisha kukabidhi ndugu Kwa taratibu za mazishi.

Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani limetoa wito kwa makampuni na taasisi za kifedha kufuata utaratibu wa kisheria katika kudai fedha kutoka kwa wateja wao ili kuepusha usumbufu  na madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo uharibu wa mali,kujeruhi na kifo.


No comments