HEADER AD

HEADER AD

ALLY HAPI MGENI RASMI UZINDUZI KAMPENI ZA CCM KAGERA

Na Alodia Dominick, Bukoba 

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kagera kinatarajia kutambulisha wagombea wake wanaotarajiwa kushiriki kinyanganyiro katika uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na kuzindua kampeini za uchaguzi huo kimkoa Novemba 20,mwaka huu.

Katibu Siasa Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kagera Hamimu Mahamud akizungumza na vyombo vya habari Novemba 19, 2024 amesema kuwa, uzinduzi pamoja na kuwatambulisha wagombea wa chama hicho watakaoshiriki kinyanganyiro cha serikali za mitaa itafanyika Novemba 20,2024 katika viwanja wa shule ya msingi Kashai.

      Katibu Siasa, Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Kagera , Hamimu Mahamud akizungumza na waandishi wa habari mkoani Kagera juu ya uzinduzi wa kampein ya uchaguzi wa serikali za mitaa na kuwatambulisha wagombea

Mahamud amesema katika uzinduzi huo, mgeni rasmi atakuwa ni katibu mkuu wa jumuiya ya wazazi Tanzania Ally Hapi akishirikiana na viongozi wa chama mkoa wa Kagera.

Aidha amesema baada ya kuzindua ngazi ya mkoa pia watazindua ngazi ya wilaya.

Amesema kuwa, katika uzinduzi huo watazungumzia mafanikio ya chama cha mapinduzi CCM kwa kipindi cha miaka minne na kuwa watapiga kampein za kistaarabu.

Ameongeza kuwa CCM imesimamisha wagombea kwa asilimia 100 na idadi yao itatajwa kesho siku ya uzinduzi na kuwatambulisha wagombea.

Aidha Mahamud amewaalika wananchi wote wa mkoa wa Kagera kuhudhuria uzinduzi huo na kuwasikiliza viongozi wa chama hicho.


No comments