KATIBU MWENEZI CCM WILAYA YA MASWA AFARIKI
Na Samweli Mwanga , Maswa
KATIBU Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu, Sitta Mashala amefariki dunia leo hii majira ya saa 12.45 jioni katika Hospitali ya wilaya ya Maswa wakati akipatiwa matibabu.
Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Simiyu,Mathias Lumeni amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na mwili umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya wilaya hiyo.
Taarifa kamili juu ya kifo hicho na taratibu za mazishi zitatolewa baadaye na uongozi wa CCM wilayani humo.
Post a Comment