MGANGA MKUU TARIME ASEMA HALI YA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI IMEPUNGUA
Na Dinna Maningo, Tarime
MGANGA mkuu wa halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Amin Vasomana amesema hali ya ugonjwa wa ukimwi katika halmashauri ya wilaya ya Tarime imepungua kutoka asilimia 1.7 mwaka jana hadi asilimia 1.5 mwaka huu.
Amesema idadi ya waathirika wa Ukimwi ni 3584 na kwamba wanaotumia dawa ni 3443 sawa na asilimia 96% wanatumia dawa.
Akijibu maswali aliyoulizwa na Mwandishi wa habari wa DIMA Online, Mganga huyo ameeleza sababu ya kupungua kwa maambukizi pamoja na changamoto.
Mwandishi : Vipi hali ya ugonjwa katika halmashauri ya wilaya y Tarime?
Mganga mkuu : Hali ya ugonjwa wa ukimwi katika halmashauri ya Tarime DC ni 1.5, maambukizi yanapungua na
sababu inayopelekea kupungua kwa maambukizi ni upimaji wa mara kwa mara unaofanyika
" Wateja wote wapya wanaopatikana wanaanzishiwa dawa, pia kufanya uchunguzi wa magonjwa ya zinaa na kuyatibu yanapobainika.
Mwandishi : Je ni kwa namna gani watu uhamasika kupima kwa hiari maambukizi ya virusi vya UKIMWI?
Mganga mkuu : Watu wanahamasika kujitokeza kupima VVU kwa hiari kwa sababu watu wengi wana huruka ya kutaka kujua afya zao.
Mwandishi : Je unafikiri ni kwanini baadhi ya watu wanaogopa kupima HIV ?
Mganga mkuu : Watu huogopa kupima VVU kwa sababu wanaogopa wakigundulika watanyanyapaliwa na jamii.
Mwandishi: Je unafikiri ni kwanini baadhi ya wagonjwa wenye virusi vya UKIMWI hukatisha dozi ya dawa ?
Mganga mkuu : Baadhi ya wagonjwa hukatisha matumizi ya dawa kwa sababu ya imani za kuombewa,
matumizi ya dawa za kienyeji na wengine kukata tamaa na kujiona ni wakufa tu.
Mwandishi: Ni kwa namna gani dawa za kurefusha maisha zimeweza kuwasaidia waathirika wa ukimwi.
Mganga mkuu : Dawa za kurefusha maisha zimewasaidia waathirika kwa kuongeza kinga na kupunguza idadi ya VVU mwilini. Unyanyapaa umepungua kwa kiasi kikubwa
Mwandishi : Ni changamoto gani mnazozipata katika kukabiliana na janga hili la UKIMWI kwa jamii?
Mganga mkuu : Uhamasikaji mdogo kwa wanaume kujitokeza kupima, uasi wa dawa , kuhama hama kwa wateja kunapelekea kushindwa kuwafuatilia
baadhi ya nyakati kuna kuwa na uhaba wa upimaji toka MSD.
Mwandishi : Nini maoni yako katika kutokomeza ugonjwa wa UKIMWI?
Mganga Mkuu: Nawaomba wananchi wawe mstari wambele kuhamasisha jamii inajikinga na matumizi sahihi ya dawa na kondomu.
Pia elimu itolewe kwa jamii kuhusu kujikinga na matumizi sahihi ya dawa za kufubaza, kuwaaelimisha ufuasi mzuri wa dawa kuhakikisha dawa na vitendanishi vinapatikana kila wakati .
Post a Comment