RC SHINYANGA AWATAKA WENYEVITI WALIOCHAGULIWA KUWASOMEA WANANCHI MAPATO NA MATUMIZI
Na Suzy Butondo, Shinyanga
MKUU wa mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha amewataka viongozi waliochaguliwa wasiende kinyume na utaratibu wa serikali kwani wakifanya hivyo serikali haitasita kuwaondoa madarakani.
Amewataka waondoe changamoto ya kutosoma mapato na matumizi kwenye maeneo yao.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha akizungumza na wenyeviti na wajumbe waliochaguliwa wa manispaa ya Shinyanga baada ya kuapishwa
Hayo ameyasema leo kwenye mkutano maalumu wa kuapishwa viongozi waliochaguliwa wa serikali ya mitaa, huku akiwataka wakurugenzi wa halmashauri sita za mkoa kuwapatia mafunzo ya uwajibikaji viongozi hao na kuwataka kuondoa changamoto ya kutosoma mapato na matumizi kwenye maeneo yao.
Macha amesema baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa wamekuwa wakilalamikiwa kutosoma mapato na matumizi, hivyo ni vizuri waliochaguliwa kuwasomea mapato na matumizi wananchi.
Wenyeviti wa mitaa na wajumbe wa kata zote za manispaa ya Shinyanga wakiapa mbele ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha
" Uchaguzi wa Serikali za mtaa umekwisha, hivyo mkawe na umoja wa kushirikiana katika kazi ili muwatumikie wananchi.
"Niwaombe sana viongozi mhakikishe kuwepo amani kwenye maeneo yenu kwani bila amani hakuna uongozi katika serikali, na kila mmoja apate miongozo ya nakala ya kusoma ili muweze kufanya rejea katika kazi zenu" amesema Macha.
Aidha mkuu wa mkoa Macha amewataka viongozi hao washirikishe na vyombo vya usalama katika ulinzi na kuwatambua wananchi kwenye maeneo wanayowaongoza, ili kuwafahamu wanafanya shughuli gani.
Wenyeviti wa mitaa na wajumbe wa kata zote za manispaa ya Shinyanga wakiapa mbele ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha
"Kila Mtaa,Vitongoji na vijiji kuna Shughuli au miradi zinazofanywa, hivyo w
mhakikishe mnakuwa walinzi wa Miradi iliyotekelezwa au inayoendelea kutekelezwa, mfano ujenzi wa Shule au Zahanati"amesema.
"Ninyi viongozi mhakikishe mnalinda migogoro ya ardhi na kuiepuka, kwani ilikuwepo changamoto ya muingiliano kati ya mtendaji au mwenyekiti kila mmoja anamajukumu yake, hivyo mshirikishane na kupeana majukumu na kuwatumikia wananchi "amesema Macha.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Shinyanga Alexius Kagunze amesema kulikuwa na mitaa 57,Vijiji 17 na Vitongoji 84 na maeneo karibu yote wamepita chama cha Mapinduzi isipokuwa kitongoji kimoja ndiyo ameshinda aliyekuwa mgombea wa Chadema.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Issa Mkondo na mwenyekiti wa Mtaa Bugweto A Mary Makamba wamesema watawatumikia wananchi wote hawataangalia kabila wala dini na suala la ulinzi na usalama watahakikisha kutojipatia fedha kwa njia isiyohalali na kuwatumikia wananchikatika kutatua shida zao.
Wenyeviti wa mitaa na wajumbe wa kata zote za manispaa ya Shinyanga wakiapa mbele ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha.
Post a Comment