HEADER AD

HEADER AD

MGOMBEA CHADEMA : MKINICHAGUA NITAKOMESHA WIZI MAJUMBANI MTAA WA MTAKUJA B

 


Na Jovina Massano, Musoma

MGOMBEA  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nafasi ya Mwenyekiti wa mtaa wa Mtakuja B, Kata ya Mwisenge, Manispaa ya Musoma mkoani Mara ,Venance  Bujwiga Chumwi
amewaomba wananchi kumchagua ili adumishe amani kwa wakazi wa eneo hilo kwani  wizi wa majumbani umekithiri  katika mtaa huo.

Akinadi sera zake amesema Mwenyekiti aliepita amekuwa akikumbatia  wanaofanya uharifu wa kuiba majumbani mwa watu kwa kupewa kitu kidogo huku jamii anayoiongoza ikipata shida kwa kuibiwa Mali zao.

       Venance Bujwiga Chumwi mgombea wa Mtakuja B Kata ya Mwisenge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA)

"Hivi Sasa Wananchi wanalazimika kuingiza mifugo ndani wakihofu kuibiwa huku mabanda ya mifugo yakiwa hayana mifugo nyakati za usiku .

" Hali hiy inaweza kuwasababishia matatizo ya kiafya hapo baadae, mkumbuke kuwa kazi kubwa ya Mwenyekiti ni kupanga maendeleo ya wananchi anaowaongoza na kushirikiana nao  si kuwatawala kwa kuwatisha kwa nafasi yako", amesema Venance.

Ameongeza kuwa katika eneo hilo kuna wajasiriamali ambao wapo kwenye eneo lisilo rasmi kibiashara na ni hatarishi hivyo ameomba wamchague ili maeneo tengefu yafanyiwe utaratibu wa kuwaruhusu wajasiriamali hao kufanyia shughuli zao katika maeneo hayo kwa usalama.

        Venance Bujwiga Chumwi mgombea wa Mtakuja B Kata ya Mwisenge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA)

Hakusita kuongelea kero ya baadhi ya miundombinu ya barabara za mtaa zisizopitika kwa kuzitolea taarifa kwa wahusika ili wakazi wanaozitumia kupata huduma kwa urahisi za usafiri.

Mbali na changamoto hizo bado mtaa huo una maeneo ambayo hayajarasimishwa na wananchi wamejenga makazi  yao na walishalipia gharama za urasimishwaji lakini Mwenyekiti aliekuwepo hajawahi kuwasaidia wananchi wake kupata haki yao ya umilikishwaji.

Kwa upande wake Ouko Fredrick mkazi wa mtaa huo amesema wanahitaji viongozi wanaotambua vema mtaa na kuwasaidia wananchi kutatua kero zao bila upendeleo na awe muwajibikaji kwa wote.

        Ouko Fredrick mkazi wa mtaa wa Mtakuja B

Nae Eliza  Sryvesta Kusaga mkazi wa Mtakuja B, amesema wakazi wa eneo hilo hasa wajasiriamali wanaofanya biashara katika eneo la makazi ya watu.

"Sisi wajasiriamali tunaomba kiongozi atakaepitishwa ajitahidi tupate eneo rasmi kwa ajili ya shughuli zetu za ujasiriamali ili tuweze kukuza biashara zetu na kujipatia maendeleo .
Eliza Sryvesta mkazi wa mtaa wa Mtakuja B

"Pia kukuza uchumi wetu kwani wengi wetu hapa tunauza mboga za majani,samaki,dagaa na vitafunwa kwa maana ya vitumbua na maandazi", amesema Eliza.

Muse Samson Masunga mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kata ya Mwisenge amesema viongozi waendelee kunadi sera zenye mashiko na tija zenye kuwalenga wananchi wa eneo husika na si Lugha za matusi kama zinavyotolewa na baadhi ya wagombea wa Chama cha Mapinduzi katika mitaa hiyo.
           
Wananchi wa Mtakuja B pamoja na wanachama wakisikiliza sera kwa mgombea wa mtaa huo

Wananchi wa Mtakuja B pamoja na wanachama wakisikiliza sera kwa mgombea wa mtaa huo

Wananchi wa Mtakuja B pamoja na wanachama wakisikiliza sera kwa mgombea wa mtaa huo

No comments