HEADER AD

HEADER AD

VITUO VYA AFYA ZAIDI YA 485 VYAJENGWA NCHINI

Na Alodia Dominick, Bukoba

VITUO vya afya zaidi ya 485 vimejengwa hapa nchini vyenye uwezo wa kufanya upasuaji zikiwemo wodi za mama kujifungua.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wazazi Taifa wa Chama cha Mapinduzi CCM Ally Hapi, wakati akizindua kampeini za uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji mkoa wa Kagera pamoja na kutambulisha wagombea wa CCM.

Katibu mkuu wa jumuiya ya wazazi Taifa Ally Hapi akizungumza na wanachama wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Kagera wakati wa uzinduzi wa kampeini za uchaguzi wa serikali za mitaa, uzinduzi umefanyika viwanja vya shule ya msingi Kashai Bukoba mjini.

Ally amesema kuwa, akina mama walikuwa wanahangaika kutafuta huduma za afya katika hospitali za wilaya, vituo vya afya vilikuwa havitoshi baada ya serikali inayoongozwa na Samia Suluhu Hassan imejenga vituo hivyo nchi nzima.

Aidha ametaja huduma nyingine zilizoboreshwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa, miundombinu ya barabara, usambazaji umeme, miradi mikubwa kama ujenzi wa reli, bandari pamoja na miradi ya maji.

"Hospitali za wilaya zimejengewa wodi nzuri za mama na mtoto, hospitali zina chumba maalumu cha wagonjwa wa dharula hiyo ni kazi ambayo imefanywa na rais wetu" amesema Ally.

Amesema kuwa, waichague CCM ndicho chama chenye viongozi wazuri,chenye sera nzuri za kuwaunganisha watu siyo sera za kuwabagua watu kwa ukanda, udini, ukabilia na ndicho chama cha kutetea masrahi ya watanzania hivyo akawataka kuchagua viongozi wanaotokana na chama hicho.

       Wanachama wa CCM waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeini za serikkali za mitaa pamoja na kuwatambulisha wagombea wa chama hicho.

Naye mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Stephen Byabato amesema miradi yenye thamani ya zaidi ya bilioni 60 imetekelezwa katika manispaa hiyo na nyingine inaendelea kutekelezwa.

Amesema wananchi wapige kura kwa wagombea wa serikali za mitaa wanaotokana na CCM ili kuweka mawasiliano mazuri kupitia chama hicho kuanzia ngazi ya chini ya mtaa, vitongoji na vijiji hadi ngazi za juu.




"Tunapofanya ufunguzi wa kampeini za serikali za mitaa tunatarajia ushindi wa  asilimia zaidi ya 100 kwa Bukoba mjini kwa sababu wagombea wetu wako shapu" amesema Byabato.

Aidha mbunge viti maalumu Neema Lugangira amesema kuwa, Bukoba mjini wanao wagombe wa CCM ambao mitaa yao haina wagombea wa vyama pinzani ipatayo 38 huku mitaa 28 ikiwa na upinzani.


Lugangira amesema katika mitaa ambayo ina upinzani watahakikisha wanapiga kampeini na mitaa hiyo wagombea wa CCM waweze kupata ushindi.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Nazir Kalamagi amesema mkoa wa Kagera una wilaya nane, kata 192, vijiji 662, mitaa 66 pamoja na vitongoji 3,664.


No comments