MADEREVA 259 WAFIKISHWA MAHAKAMANI KATI YAO 63 WAFUNGIWA LESENI
Na Alodia Dominick, Bukoba
KAMANDA wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera , Blasius Chatanda amesema ajali za barabarani zimepungua kutoka ajali 56 mwaka 2023 hadi ajali 45 mwaka 2024.
Akizungumza na waandishi wa habari Desemba, 24,2025 Kamanda huyo amesema kwa sasa jeshi hilo limedhibiti ajali za barabarani kwa kiasi kikubwa na kufanikiwa kuzipunguza ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua mbalimbali za kisheria, kuwafikisha mahakamani.
"Jumla ya madereva 259 walifikishwa mahakamani kati yao madereva 63 wamefungiwa leseni kwa kipindi cha Kuanzia miezi mitatu hadi miaka mitatu kwa makosa ya mwendo kasi, ulevi, kuzidisha abiria, wengine wamehukumiwa kugungwa jela miezi mitatu hadi miaka mitatu" amesema Chatanda
Ameeleza kuwa madereva 178 walipewa adhabu ya kulipa faini mahakamanina madreva tisa wa mabasi wamefungiwa leseni zao kwa kosa la mwendo kasi.
Pia ameeleza kuwa, pamoja na mapambano hayo dhidi ya ajali za barabarani lakini kwa mwaka huu kuna matukio makubwa mawili ya ajali yaliyosababisha vifo vya watu 18 na majeruhi zaidi ya 25 ambayo yalisababishawa na uzembe wa madereva.
Amesema, moja ya ajali hizo ilitokea Desemba 03, 2024 katika maeneo ya kizuizi cha barabarani cha ukusanyaji wa ushuru wa mazao kilichopo kata ya Kihanga wilaya ya Karagwe katika barabara kuu ya rami itokayo Karagwe kwenda Misenyi mkoani Kagera.
Gari lenye namba sa usajili T 472 EAQ lenye trela namba T621 EJQ aina ya scania mali ya molemeta kampani limited iliyogonga kwa nyuma magari mawili ya abiria yenye namba za usajili T 367 ECP aina ya mitsubishi Rosa na T 976 DGD aina ya toyota haice na kusababisha ajali na kusababisha vifo vya watu saba.
Waliofariki katika ajali hiyo wanawake walikuwa wanne, watoto wawili, mwanaume mmoja na majeruhi tisa.
Ajali nyingine imetokea Desemba 21,mwaka huu katika kijiji cha Kabukome kata na tarafa ya Nyarubungo wilaya ya Biharamlo katika barabara kuu ya Biharamlo kwenda Muleba.
Amesema, gari lenye namba za usajili T857 DHW Scania basi mali ya Roja line travel company Ltd likiendesha na Said Mkenda (41) likitokea mkoani Kigoma kwenda Bukoba dreva huyo alisimama kushusha abiria ambaye alikuwa mtoto aliyepitilishwa kwenye kituo.
"Gari lilisima ila lilishindwa kupanda mlima na kurudi nyuma kisha kuingia mtaloni na kupinduka na kusababisha vifo 11 na majeruhi 16 katika vifo hivyo wanawake walikuwa sita, wanaume watano" amesema Chatanda.
Amesema, jeshi hilo kupitia kitengo cha usalama barabarani linaendelea kuhamasisha na kutoa elimu endelevu ya usalama barabarani kwa umma kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hususan vyama vya waendesha pikipiki (bodaboda) wasafirishaji, shule za msingi na sekondari na vyombo vya habari.
Katika kutoa elimu wametumia redio za kijamii za mkoani Kagera zipatazo tisa kila wiki vipindi vinne, jumla ya shule zilixopstwa elimu 2,413 na vituo vya waendesha pikipiki 7,975.
Post a Comment