HEADER AD

HEADER AD

MAONESHO YA UWEKEZAJI KUFANYIKA PWANI


Na Gustaphu Haule, Pwani

MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ametangaza kufanyika kwa maonesho makubwa ya uwekezaji na biashara yatakayoanza Desimba 16 hadi Disemba 20 mwaka huu katika viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mjini.

Kunenge ametoa taarifa hiyo Disemba, 2, 2024  katika mkutano wake na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali uliofanyika ofisini kwake iliyopo Mjini Kibaha.

     Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge, akizungumza na waandishi wa habari  Desemba 02 kuhusu maonesho ya uwekezaji na biashara yanayotarajia kuanza Desemba 16 hadi Desemba 20 mwaka huu katika viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mjini.

Katika kikao hicho Kunenge amesema kuwa maonesho hayo kwa mkoa wa Pwani ni ya nne kufanyika kwani kwa mara ya kwanza yalianza kufanyika mwaka 2018,2019 ,2022 na sasa yatafanyika 2024.

Amesema maonesho hayo yatafunguliwa Desemba 17 na yanatarjiwa kuwa na washiriki 550 huku akiomba wananchi kujitokeza kutembelea maonesho hayo kwa ajili ya kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa katika mkoa wa Pwani.

        Moja ya kongamano la uwekezaji na biashara lililowai  kufanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha kwa Mfipa Mkoani Pwani

Kunenge amesema lengo kubwa la maonesho hayo ni kutangaza fursa za uwekezaji, kufungua fursa za masoko na kutangaza bidhaa mbalimbali zinazozalishwa Mkoa wa Pwani .

"Maandalizi ya maonesho hayo yanakwenda vizuri na mkoa umejipanga kuhakikisha maonesho hayo yanafanyika Kwa ufanishi mkubwa kwani tutakuwa na wafanyabiashara wakubwa na wa kati ,taasisi wezeshi za Serikali na binafsi hivyo ni fursa kwa kila mtu kujifunza na hata kupata fursa za uwekezaji,"amesema Kunenge 

Aidha, Kunenge amesema kuwa katika wiki ya maonesho hayo Disemba 18 kutakuwa na kongamano kubwa la wafanyabiashara na wawekezaji litakalofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha kwa Mfipa.

"Desemba 18 mwaka huu tutakuwa na kongamano kubwa la wafanyabiashara na wawekezaji ambapo litahudhuliwa na washiriki wapatao 400 zikiwemo taasisi za Serikali na binafsi,"amesema Kunenge.

Kunenge ameongeza kuwa mkoa wa Pwani mpaka sasa kuna viwanda 1,553 lakini tangu Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, mkoa wa Pwani umepata viwanda vikubwa 78 ambapo mkoa umenufaika zaidi.

Hata hivyo, Kunenge ameendelea kuwaomba wadau mbalimbali kuja kushiriki maonesho hayo kwakuwa itawasaidia kupata ushauri kutoka kwa wadau wengine,kujifunza zaidi na hata kuuza bidhaa zao .

         Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu RIdhiwani Kikwete akiwa katika moja ya maonesho ya biashara na uwekezaji yaliyowai kufanyika Mkoani Pwani.

No comments