MKURUGENZI KAMPUNI YA RIN AKABIDHI MILIONI NNE CHAMA CHA WASIOONA TARIME
>>Awali alichanga Tsh Milioni moja zikabaki Milioni nne, ametekeleza ahadi
Na Dinna Maningo , Tarime
MKURUGENZI wa kampuni ya ujenzi ya RIN , Isaack Range, mkazi wa Kijiji cha Nyangoto -Nyamongo ,wilayani Tarime, amekabidhi Tsh Milioni nne kwa Chama cha Wasioona wilaya ya Tarime (TLB) mkoani Mara ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake aliyoiahidi wakati wa changizo.
Novemba, 29, 2024, Mkurugenzi huyo wa kampuni ya RIN alichangia Tsh. Milioni moja keshi na kuahidi kutoa milioni 4 Desemba, 06, 2024 ambapo ametekeleza ahadi na hivyo kuchangia Tsh. Milioni tano.
Changizo hilo liliendeshwa na mkuu wa wilaya ya Tarime , Meja Edward Gowele aliyekuwa mgeni rasmi kuwakabidhi fimbo nyeupe na miwani wanachama wa chama cha wasioona wilayani humo.
Msaada uliotolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya WARACHA ,Daud Ryoba Tindo, alitoa fimbo 58 zilizonunuliwa kwa thamani ya Tsh. 1,400,000 na miwani 5 yenye thamani ya Tsh. 400,000 ambapo pia Daud alichangia Tsh.500,000 na kufadhili gharama za usafiri kwa wasioona 45 walioshiriki katika hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele akipokea fimbo nyeupe na miwani kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ujenzi na usambazaji wa bidhaa mbalimbali WARACHA, Daud Tindo (kulia) ili kuwakabidhi Wasioona wilaya ya Tarime
Pia wadau mbalimbali walimuunga mkono mkuu huyo wa wilaya na hivyo kufanikiwa kupatikana kiasi cha Tsh. 3, 335, 000 na ahadi zaidi ya Tsh. Milioni 5
Baadhi waliochanga ni pamoja na Diwani mstaafu Agustino Sasi mkazi wa Kijiji cha Kewanja-Nyamongo alichanga Tsh. 200,000 huku akimshukuru mkuu huyo wa wilaya kufika kujumuika na wasioona.
Mkazi wa Kijiji cha Nyangoto John Jonathani alichanga Tsh. 500,000 na kusema ndio mara yake ya kwanza kualikwa kwenye shughuli za watu wenye ulemavu wa macho.
Wengine waliotoa michango yao ni Josephati Mwita ametoa Tsh.300,000 na kufadhili maji na soda kiasi cha Tsh.170,000 wakati wa kikao hicho. Mkurugenzi wa hoteli ya Silver Spring, Godfrey Kubyo amechangia Tsh. 500,000 pamoja na kufadhili chakula.
Kampuni ya KEMANYANKI imetoa Tsh. 150,000, Julias Orindo mzazi wa mtunza hazina TLB ametoa Tsh. 200,000, Winers Tsh. 100,000 , Mchungaji Doto Shija wa kanisa la waadventista wasabato Nyamongo kati Tsh. 100,000 na wengine waliahidi kutoa michango yao ifikapo Desemba, 6, 2024 .
Mwenyekiti wa Chama cha wasioona mkoa wa Mara, Nyamlanga Rwakatare amemshukuru mkuu wa wilaya ya Tarime na wadau wa maendeleo kukutana nao na kuwachangia fedha.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele akimkabidhi fimbo nyeupe Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona mkoa wa Mara , Nyamlanga Rwakatare (TLB), fimbo hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya WARACHA.
" Hii ni shughuli ya kwanza mkoani kwetu Chama cha wasioona kupewa fimbo nyeupe na miwani. WACHA tunakupongeza sana , tunaomba wadau wengine waendelee kutusaidia WARACHA pia endelea kutusaidia" amesema Nyamlanga.
Mtunza hazina wa Chama cha wasioona wilaya ya Tarime, Bhoke Jonathan ambaye amekuwa mstari wa mbele kutafuta wafadhili kufadhili vikao na vifaa kwa ajili ya wasioona amemshukuru mkuu wa wilaya kwa kufika kushirikiana nao na wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakiwasaidia ikiwemo Kampuni ya KEMANYANKI.
Mkuu wa wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele akipokea zawadi ya kitenge ya mkewe kutoka kwa Bhoke Orindo kilichotolewa na Chama cha wasioona Tarime
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya WARACHA, Daud Tindo akizungumza wakati wa halfa ya kukabidhi fimbo nyeupe kwa watu wasioona
Wasioona wakiwa kwenye hafla ya kupokea fimbo nyeupe zilizotolewa na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya WARACHA, Daud Tindo
Post a Comment