HEADER AD

HEADER AD

TCRA : WANAOMILIKI VYOMBO VYA HABARI BILA KUWA NA LESENI KUKIONA


 Na Jovina Massano, Musoma

MENEJA wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salumu         amewataka Waandishi wa habari wanaomiliki vyombo vya habari mkoa wa Mara kurasimisha  vyombo vyao kwa mujibu wa Sheria.

Ameyasema hayo wakati warsha ya siku moja katika ukumbi wa mwembeni complex uliopo Manispaa ya Musoma kwa wamiliki wa vyombo vya habari na waandishi wa habari kuwakumbusha kuhusu kanuni za leseni .

        Meneja wa mamlaka ya mawasiliano Kanda ya ziwa mhandisi Imelda Salum

"Mamlaka ya mawasiliano imeona kuna umuhimu wa kuwapa uelewa wadau wetu wa nini mamlaka inafanya kwenye usimamizi wa sekta yetu ya utangazaji hususani eneo la maudhui hasa ya kwenye mtandao" amesema.

Ameongeza kuwa wale wanaojishughulisha na kazi za kihabari mitandaoni pasipokuwa na leseni wachukue hatua stahiki za kuomba leseni ili waweze kufanya shughuli zao wakiwa wanatambuliwa na kufahamika.

Amesema itasaidia kupata msaada wanapohitaji kutoka mamlaka ya mawasiliano kwa kuwa inafanya kazi na wadau wanaotambulika.

Ameongeza kuwa upatikanaji wa leseni hivi sasa umeboreshwa mteja anaweza kuomba leseni kwa njia ya mtandao kidigitali.

         Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo

Amekumbusha kuwa, kwa mujibu wa Kanuni ya Maudhui Mtandaoni ya mwaka 2020 kifungu 4(1) Mtu yeyote hatatoa maudhui mtandaoni bila kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Adhabu ya mtu anayepatikana na kosa la kutoa maudhui mtandaoni bila leseni ni faini isiyopungua milioni 5 au kifungo kisichopungua mwaka mmoja kwa hiyo wale wanaotoa habari mitandaoni na hawajasajiliwa hilo ni kosa kisheria.

Mwenyekiti wa chama cha Waandishi wa habari mkoani hapa Jacobo Mgini, amewahimiza wamiliki wote wanaotoa maudhui mitandaoni kufuata kanuni na sheria za mamlaka ya mawasiliano ili kuiheshimisha tasnia ya habari hapa nchini.

        Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Mara Jacobo Mgini

"Ni wakati muafaka sasa wa kusajili vyombo vyao ili kuweka heshima kwani mkoa wa Mara una vyombo vingi vinavyotoa maudhui mitandaoni lakini kwa mujibu wa meneja wa mawasiliano Kanda amebainisha vyombo saba pekee ndivyo vilivyo hai",amesema Jacobo.

Nae Mwandishi wa habari, Ada Shadrack amempongeza mmiliki wa  DIMA Online kuwa mojawapo ya vyombo vyenye leseni hai katika mkoa huu wa Mara.

Kwa mujibu wa Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa vyombo vya habari vya mtandaoni vilivyosajiliwa ni saba ikiwemo DIMA Online, Mara Online News, Lake Zone Watch, George Marato TV, Kitaji Ndoto Yetu Initiative na Cleo Online TV.
           


No comments