WANANCHI WAISHUKURU KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA KUWAPA ELIMU YA SHERIA
Na Jovina Massano, Musoma
WAKAZI wa mtaa wa Mtakuja A Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, wameshukuru uwepo wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia kuwafikia kuwapa elimu ya sheria.
wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwasaidia kupata elimu ya sheria bila gharama ambayo imewafikia mahali walipo .
Wakazi wa mtaa wa Mtakuja A Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma wakiwasikiliza wataalam wa Sheria ikiwa ni mojawapo ya njia za kupata uelewa wa kisheria
Wananchi wametoa shukrani hizo kwa mratibu wa kampeni ya mama Samia mkoa wa Mara, Laurent Burilo wakati wa mkutano wa hadhara wa mtaa huo uliofanyika jirani na mnara wa Halotel ambapo wananchi wameweza kupata elimu ya Sheria ya masuala mbalimbali ya mirathi, ndoa, ardhi na masuala ya ukatili.
Peter Nyarufunjo mkazi wa mtaa wa Mtakuja A ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi mahili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuja na mpango madhubuti wa kuwapa uelewa wa kisheria wananchi wake kwa kuwafikia hadi wa ngazi za chini.
Peter Nyarufunjo mkazi wa mtaa wa Mtakuja A Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma
"Kwanza tunampongeza mratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia kwa kukubali kufika katika mtaa huu na jopo lake la sheria kwa kutoa elimu hii.
"Jamii yetu kwa kiasi kikubwa ina changamoto ya mirathi, ndoa na migogoro ya ardhi sana ardhi kesi zinachukua muda mrefu hatuelewi tatizo ni nini, tunaomba hili liangaliwe kupunguza kero hii", amesema Peter.
Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia imelenga kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu masuala ya haki zao, sheria, na haki za binadamu yanayojumuisha changamoto zilizopo Kwenye jamii.
Afisa Uchunguzi mkuu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, ambaye pia ni Mratibu wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) na Mratibu wa kampeni mkoani hapa Laurent Burilo, ameeleza kuwa kampeni imelenga kuongeza uelewa kwa wananchi kujusu suala la haki zao na upatikanaji haki kwa wakati na wajibu wao.
Katika mkoa huu kampeni hiyo imefika katika halmashauri zote na kila halmashauri imelenga kata kumi na kila kata wamefikia vijiji vitatu au mitaa mitatu na kuweza kufikia vijiji 270.
Pia imewaunganisha wananchi na wanasheria ambao watatoa huduma za kisheria bure na hata mahakamani watawasimamia bila malipo.
Mbali na hayo kampeni inatoa utatuzi wa kisheria unatolewa sambamba na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa huduma za kisheria.
" Ni azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwasaidia wananchi wanyonge kuhusu masuala ya haki zao na wajibu wao na upatikanaji wa haki kwa wakati",amesema Laurent.
Wakili wa kujitegemea kutoka chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) Emanuel Baraka, amesema changamoto kubwa ni migogoro ya ardhi inayopelekea uwepo wa kesi nyingi huku zikishindwa kutatuliwa kwa wakati kwakuwa zinatatuliwa na Mwenyekiti peke yake, na kulemewa na kesi , hivyo kupelekea kuchukua muda mrefu kutatuliwa.
Wakili wa kujitegemea kutoka Chama Cha mawakili Tanganyika (TLS)Mkoa wa Mara Emmanuel Baraka akijibu maswali katika mkutano kwa wakazi wa mtaa wa Mtakuja A Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
"Kama inavyofahamika mabaraza ya ardhi na nyumba hapa nchini yapo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria, ndio mwenye wajibu wa kuongeza wenyeviti kupitia msajili wa mabaraza akishauriana na Waziri wa ardhi na nyumba," amesema Baraka.
Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa haliendaa mkutano huo Aloyce Masatu Lawi maarufu Kayolla, amesema lengo la mkutano huo ni kuwasaidia na kuwafikishia wakazi wa mtaa huo elimu ya kisheria.
Mwenyekiti wa mtaa wa Mtakuja A Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma mkoani Mara Aloyce Masatu Lawi maarufu Kayolla
Pia amewashukuru wananchi kwa kumwamini na kumchagua tena kuendelea kuwa mwenyekiti kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27,2024.
"Maendeleo bila amani haki hakuna hivyo ninaipongeza Wizara ya Katiba na Sheria kwa usikivu wao na kufanikisha azma ya Rais wetu kuwajengea wananchi uelewa wa kisheria.
Post a Comment