HEADER AD

HEADER AD

POLISI SHINYANGA WAKAMATA SILAHA AINA YA GOBORE IKISAFIRISHWA KWA BAISKELI

>> RPC Shinyanga aeleza mafanikio 

Na Suzy Butondo , Shinyanga

JESHI  la Polisi mkoani Shinyanga limekamata silaha aina ya Gobore katika kijiji cha Bugomba A, Kata ya Ulewe Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani hapa, ikiwa imepakiwa kwenye baiskeli, huku mtuhumiwa akikimbia mara baada ya kuona gari la polisi.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya  habari Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi, amesema kufuatia misako na Operesheni mbalimbali ambazo wamezifanya  kuanzia novemba 27 hadi Desemba 22, 2024, kwa lengo la kubaini na kuzuia uhalifu kwa kukamata wahalifu wa makosa mbalimbali.


    Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akitoa taarifa kwa vyombo vya habari

Magomi amesema katika msako na operesheni hiyo, jumla ya watu 81 wamewakamata na vielelezo mbalimbali, ikiwamo silaha aina ya Goboremadini bandia gramu 250 yadhaniwayo kuwa ni dhahabu.

Pia bangi gramu 9,000, mirungi bunda tisa, Gongo lita 113,Sola panel saba,betri Nne za Sola, pikipiki 11,kadi tatu za pikipiki,Antena nne za Ving'amuzi.

Vingine ni redio mbili, baiskeli mbili,mashine moja ya bonanza,kamera moja, na mitambo minne ya kutengeneza Gongo.

Amesema kwa upande wa makosa ya usalama barabarani,wamekamata makosa 5,376, Magari 3,767, Bajaji na Pikipiki 1609, na wahusika waliwajibishwa na kulipa faini za papo kwa papo.

"Katika mafanikio ya kesi mahakamani  jumla ya kesi 18 zimepata mafanikio ambapo kesi moja ya kubaka mshitakiwa amehukumiwa miaka 30 jela, kesi moja washitakiwa wanne kifungo cha maisha jela kwa kosa la unyang"anyi wa kutumia silaha na kifungo cha miaka 30 jela  kwa kumlawiti mwanamke mmoja wa kata ya Ngokolo pamoja na kunyang"anywa simu yake.

Kesi nyingine ni kumiliki nyara za serikali kinyume na sheria washitakiwa watatu wamehukumiwa miaka 17 na miezi mitano jela, kesi moja kupatikana na dawa za kulevya aina ya bhangi.

        Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
 
Mshitakiwa amehukumiwa miaka mitatu jela, kesi saba za wizi washitakiwa 12 wamehukumiwa kati ya miezi mitatu hadi miaka mitatu jela, kesi ya kujalibu kubaka mshitakiwa amehukumiwa miaka 30 jela.

"Na kesi moja ya kuvunja nyumba washitakiwa watatu wamehukumiwa miaka mitatu jela kesi moja ya kughushi mshitakiwa amehukumiwa miaka miwili jela, kesi moja kutoroka chini ya ulinzi.

" Mshitakiwa amehukumiwa mwaka mmoja jela, kesi mbili za shambulio washitakiwa wawili wamehukumiwa kati ya miezi miwili hadi mitatu jela na kesi moja kuingia kwa jinai,mshitakiwa amehukumiwa miezi mitatu jela"amesema Magomi.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu, huku akiwakumbusha wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka, wasiwaruhusu watoto kwenda kutembea nyakati za usiku.




No comments