RC KAGERA AAGIZA KITENGO CHA USALAMA BARABARANI KUKAGUA MAGARI KABLA YA SAFARI
Na Alodia Dominick, Bukoba
MKUU wa mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa amekiagiza kikosi cha usalama barabarani kufanya ukaguzi wa magari kabla ya kuanza safari kama njia ya kupunguza ajali za barabarani.
Ni baada ya kutokea ajali ya gari iliyosababisha vifo vya watu 11 na majeruhi 16 katika wilaya ya Biharamlo mkoani humo.
Ajali hiyo ilitokea jana Desemba 21,2024 saa 8:00 mchana baada ya basi la kampuni ya Copco one yenye namba za usajili T857DHW aina ya Scania inayofanya safari zake kutoka Kigoma kwenda mjini Bukoba kufeli breki wakati limesimama kumshusha abiria na kuanza kurudi kinyumeyume na kuacha njia kisha kupinduka.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa ameyasema hayo, Desemba 22, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali ofisini kwakwe mjini Bukoba ambapo amesema ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Kabukome kata Nyarubungo katika eneo la mlima Kasindaga wilaya ya Biharamulo.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake
Mwassa amesema gari lenye namba za usajili T857 DHW Scania basi mali ya Roja line travel company Ltd likiendesha na Said Mkenda (41) likitokea mkoani Kigoma kwenda Bukoba.
Ameongeza kuwa dreva alisimamisha gari kushusha abiria ambaye alikuwa mtoto aliyepitilizwa kwenye kituo, ndipo gari lilisima ila lilishindwa kupanda mlima na kurudi nyuma kisha kuingia mtaloni na kupinduka na kusababisha vifo 11 na majeruhi.
"Katika vifo hivyo wanawake sita,wanaume wanne na watoto wawili tumepokea kwa masikitiko makubwa sana ukizingatia ndani ya kipindi kifupi tumepata ajali mbili zilizochukua maisha ya watu wengi siku chache zilizopita"
Hivi karibuni ilitokea ajali mbaya wilayani Karagwe na hii ya jana, natumia fursa hii kutoa pole kwa wananchi wa mkoa wa Kagera na ndugu na jamaa waliopoteza ndugu zao"ameeleza kwa masikitiko Mwassa
Ametoa ombi kwa wananchi wa mkoa huo hasa madreva kuwa waangalifu wanapoendesha magari ya abiria na binafsi hasa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ambapo kunakuwa na ajali nyingi hivyo aliagiza polisi kitengo cha usalama barabarani kufanya ukaguzi wa magari kabla ya kuanza safari.
Pia amewataka kuhakikisha usalama na uzima wa gari na spidi zinazoendeshwa ziwe zinazoruhusiwa. Amesema, majeruhi 16 walilazwa katika hospitali teule ya Biharamulo ambapo 12 mchana huu wameruhisiwa na wanne akiwemo dreva wanandelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.
Kamanda wa polisi mkoani Kagera Blasius Chatanda, amesema uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha ajali hiyo ni ubovu wa gari hilo na uchuguzi zaidi unaendelea.
Aidha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa alifika eneo ilipotokea ajali na kuwajulia hali majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Biharamulo.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Innocent Bashungwa akiwapa pole wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Biharamlo, kulia kwake ni kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Blasius Chatanda.
Akizungumza baada ya kutembelea majeruhi jana, Waziri Bashungwa ametoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wote walioguswa na ajali hiyo na kutoa wito kwa Watanzania kuendelea kuwaombea majeruhi wapone haraka.
Naye Mganga mkuu wa hospitali teule ya Biharamulo, Dkt Gresmus Sebuyoya ameeleza kuwa majeruhi wote wanaendelea na matibabu na ungalizi wa karibu wa madaktari.
Post a Comment