SHAIRI: MUNGU TUNAKUSHUKURU NI 2025
MUNGU tunakushukuru, kwamba tumevuka mwaka,
Tumeona mpya nuru, mwaka mpya tumefika,
Ni neema si ushuru, ametujazi Rabuka,
Asante Muumba wetu, mwaka huu kuufika.
Sindwele yaliyopita, umefika mpya mwaka,
Baraka zake twachota, kwetu ziweze kufika,
Tuweze kupitapita, na kuzidi kuinuka,
Asante Muumba wetu, mwaka huu kuufika.
Tangulia mbele kwetu, kati tusije katika,
Kwa yote mipango yetu, iweze tekelezeka,
Kusiwe kilio kwetu, ila raha na kucheka,
Asante Muumba wetu, mwaka huu kuufika.
Shairi limetungwa na Lwaga Mwambande
lwagha@gmail.com
Post a Comment