HEADER AD

HEADER AD

SHAIRI : WAANDISHI WA HABARI, MKONO WENU WA HERI


WAANDISHI wa habari, kutoka Kanda ya Ziwa,

Mkono wenu wa heri, kwa kweli nawaelewa,

Mlivyovyofanya vizuri, Soko akainuliwa,

Mwenyekiti wa semina, sasa hadi MISA-TAN.


Soko wala hakupingwa, jinsi mnamuelewa,

Kumbe mtu hana nongwa, uongozi aelewa,

Kweli wengi tulijengwa, kaziye tulinogewa,

Mwenyekiti wa semina, sasa hadi MISA-TAN.


Mlishajenga msingi, njia akaandaliwa,

Na aliupiga mwingi, pasipo na kuchachawa,

Kumbe mwanzo wa udingi, kwa kura aliopewa,

Mwenyekiti wa semina, sasa hadi MISA-TAN.


Ukosoaji ujenzi, Soko anauelewa,

Si mkausha pumzi, ifike umezidiwa,

Kujenga ndiko aenzi, azidi kubarikiwa,

Mwenyekiti wa semina, sasa hadi MISA-TAN.


Heri tunamtakia, azidi kubarikiwa,

Kazi akitufanyia, na mengi kutunukiwa,

Hadi aje kufikia, kote akotabiriwa,

Kwanza shavu la semina, kisha sasa MISA-TAN.

Mtunzi wa Shairi ni Mtunzi wa Shairi ni Lwaga Mwambande (KiMPAB)

No comments