HEADER AD

HEADER AD

TNMC YAJIPANGA MTIHANI WA USAJILI, UTOAJI LESENI KWA WAHITIMU 5147


Na Gustaphu Haule, Pwani

BARAZA la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) limejipanga kuendesha mtihani wa usajili na leseni kwa wahitimu 5,147 katika vituo saba nchini utakaowahusisha wahitimu katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga hapa nchini Agness Mtawa, ametoa taarifa hiyo Desemba, 18, 2024, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi zake zilizopo Kibaha mkoani Pwani ambapo usajili na leseni utafanyika Desemba, 20, 2024.


Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania( TNMC) Agness Mtawa wa kwanza kulia akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha Desemba 18,2024,  kushoto ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Maendeleo ya Taaluma ya Uuguzi nchini Tanzania Happy Masenga.

 kuhusu kuelekea katika mtihani wa usajili na leseni kwa Wauguzi na Wakunga pamoja na wataalamu wa dawa za usingizi na ganzi utakaofanyika Disemba 20 mwaka huu.

Amesema mtihani huo hufanyika kwa mujibu wa sheria ya uuguzi na ukunga ya mwaka 2010 kifungu cha 6(0), na Kifungu cha 15 (1) (a) .

Mtawa amesema kuwa lengo la mtihani huo ni kupima umahiri kabla ya kumsajili mwanataaluma na kumruhusu kwenda kutoa huduma kwa jamii na kwamba jukumu hilo linafanyika ili kuhakikisha umma unapata huduma iliyopo bora na sslama.

"Jumla ya watahiniwa 5,147 wamekidhi vigezo vya kufanya mtihani huu,na watahiniwa hawa wanajumuisha wahitimu ngazi ya Astashahada 86, stashahada 4498,shahada ya uuguzi  537,shahada ya Ukunga 11, na shahada ya Uuguzi katika utoaji dawa za usingizi na gazi 15,"amesema Mtawa.

Katika ufafanuzi huo, ametaja vituo ambavyo Watahiniwa watafanya mtihani huo kuwa ni Tandabui kilichopo mkoani Mwanza yeye idadi ya 995,Chuo Kikuu cha Dodoma ( UDOM) Watahiniwa 429,Chuo cha SJUT Mtakatifu Yohana kilichopo Mkoani Dodoma Watahiniwa 677.

Amesema vituo vingine kuwa ni Rucu  kilichopo mkoani Iringa chenye watahiniwa 687,Chuo cha Kampala kilichopo Jijini Dar es Salaam (1313),Tabora Polytechnic kilichopo mkoani Tabora (420) na chuo cha IAA kilichopo Mkoani Arusha (626).

Mtawa ameongeza kuwa kwa mara ya kwanza Baraza hilo litatoa mtihani wa wauguzi ambao ni wataalamu wa utoaji dawa za usingizi na ganzi ambapo mtihani huo umetanguliwa na mtihani wa vitendo kwa lengo la kupima umahiri katika kutoa huduma ya dawa za usingizi na ganzi.

        Hili ni jengo la ofisi ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) lililopo Mjini Kibaha Mkoa wa Pwani.

"Watahiniwa wote wanatakiwa kufika katika vituo vyao siku moja kabla ya siku ya mtihani yaani Desemba 19,2024 ambapo kila mtahiniwa anapaswa kuwa na vifaa ikiwemo kalamu nyeusi aina ya Obama au Penseli HB, picha mbili za Passport,na kitambulisho cha NIDA,cha kupigia kura au leseni ya udereva,"amesema Mtawa

Mtawa amewakumbusha watahiniwa hao kuhakikisha wanajiepusha na tabia za udanganyifu kabla na wakati wa chumba cha mtihani kwani wakibainika kujihusisha na vitendo hivyo ni kosa .

Hatahivyo, Mtawa amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya uuguzi na ukunga ya mwaka 2010 kifungu cha 19(3) na kwa mujibu wa sheria hiyo adhabu yake ni kufutiwa mtihani kwa mujibu wa kifungu cha 22 cha kanuni.

Kwa upande wake mkurugenzi wa mafunzo na maendeleo ya taaluma ya uuguzi nchini Tanzania, Happy Masenga amesema kuwa maandalizi ya Mtihani huo yamekamilika na kinachotakiwa ni utayari wa mtahiniwa kwenye chumba cha mtihani.


No comments