CCM BUTIAMA YAWAONYA WANACHAMA WANAOJIPITISHA
Na Jovina Massano, Butiama
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Butiama, mkoani Mara, kimewaonya wanachama wanaojipitisha kwa wananchi wakifanya kampeni za kutangaza nia ya kugombea ubunge na udiwani.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya Butiama, Marwa Siagi akizungumza hivi karibuni katika kikao cha halmashauri kuu ya CCM kilichofanyika katika ukumbi wa kontena, ukiwahusisha wajumbe wa chama hicho kutoka vijiji na kata zote, amewaonya wanaojipitisha .
Marwa amesema kuwa siku za hivi karibuni baadhi ya wanachama ambao hajawataja majina yao wamekuwa wakifanya kampeni kwa lengo la kutangaza nia kugombea nafasi za uongozi jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu na miiko ya chama.
" Wapo watu walishangazwa na hiyo hali lakini kuna wengine walishabikia na wengine kuhoji kuwa hivi viongozi wapo wapi wanasikia na wamekaa kimya. Ndugu wajumbe viongozi wa chama chenu wapo macho muda wote na wako makini.
" Taratibu za chama ziko wazi mbunge yupo madarakani, madiwani wako madarakani na rais yupo madarakani lakini kuna wanachama wameanza kupita na kuanza kampeni kabla ya wakati.
" Huo ni uvunjifu wa kanuni na katiba ya chama muda bado, ukifika kwa mujibu wa chama ruksa kuomba hata ikitokea wameomba mia moja", amesema Marwa.
Ameongeza kuwa tayari kamati ya siasa imekaa kuwajadili wale walioshindwa kuheshimu taratibu za chama kwa kuonyesha dharau na kwamba tayari hatua zimeishachukuliwa ili iwe fundisho kwa wengine.
Nae Katibu wa CCM Kata ya Nyamimange Stella Petro, amesema kuwa alichokiongea Mwenyekiti ni sahihi kwani mtu anapokuwa madarakani anatakiwa aachwe afanye kazi zake bila kuingiliwa hadi muda wake wa uongozi utakapokwisha.
Katibu wa CCM Kata ya Nyamimange Stella Petro Petro akizungumza."Huu ni ukiukwaji wa katiba ya chama si busara, ni vema sasa waache waliopo madarakani wafanye kazi muda ukifika waingie ulingoni kila mtu aendelee na mambo yake",amesema Stella.
Diwani wa Kata ya Buruma Sospeter Kitenyi amesema Demokrasia inapokuwa ipo mahali itumike kwa makini na kanuni itumike ili ikitokea mtu amekwenda kinyume basi utaratibu ufuate.
Diwani wa Kata ya Buruma Sospeter Kitenyi akizungumzaAmeongeza kuwa hivi sasa hata kwenye kata watu wameshaanza kupita kutangaza nia na jambo ambalo si sahihi hivyo ni vyema kila mtu aheshimu mujibu katiba ya chama.
Post a Comment