HEADER AD

HEADER AD

MWENYEKITI MBWAMAJI AANZA NA UKARABATI WA BARABARA ZA MTAA


Mwandishi Wetu, Kigamboni
 
MWENYEKITI wa Mtaa wa Mbwamaji uliopo Gezaulole Kata ya Somangila Wilayani Kigamboni,  Yohana Luhemeja 'Maziku' ameanza kwa kishindo katika kuhakikisha anatekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) .

Ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi  ya maendeleo kwa wananchi ambapo ameendesha zoezi la  uchongaji wa barabara 8, zinazoingia na kutoka katika Mtaa huo.


Zoezi hilo lilianza jana Januari 19, 2025 la uchongaji wa barabara zenye urefu wa km.2 pamoja na kufukia madimbwi na vifusi ambavyo vilikuwa kero.

"Zoezi hili la uchongaji wa barabara linafuatia kikao changu cha kwanza nilipoapishwa tu, niliahidi kuanza na kero hii. Tumeanza rasmi Januari 19, na litafikia tamati kesho Januari 21,2025. Tumeanza na barabara hizi nane kwanza, baadae tunaendelea na zingine.

" Tunashukuru halmashauri ya Manisapaa ya Kigamboni kupitia kwa Mkurugenzi na Diwani wetu wa Kata ya Somangila kutupatia greda na sisi ofisi yetu imeweza kuratibu mafuta na nguvu kazi.

" Tumeshirikiana na Katibu wa CCM Tawi, Kamati ya Ardhi ya mtaa na kamati ya miundombinu ambazo tumefanikisha kuhakikisha. Lengo ni kuhakikisha mtaa wa Mbwamaji wananchi wanaingia na kutoka bila kero ya miundombinu.". Amesema Maziku.

Maziku ameongeza kuwa ataendelea kuwapambania wananchi wa mtaa huo ikiwemo kuwasogezea huduma muhimu za maji, afya, elimu na soko.


"Tunawashukuru viongozi wetu wa juu wa chama na serikali kwa kupeleka maendeleo ngazi ya chini, Mbwamaji tunamhakikishia Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan atapata kura za kishindo za urais. Mbwamaji ya maendeleo ipo tayari tuungane kwapamoja". amesema Maziku.

Mtaa huo wa Mbwamaji ni miongoni mwa mitaa mikongwe hapa nchini wenye historia ya kipekee ikiwemo kuwa na Kijiji cha kale, Mtaa ambao pia umezungukwa fukwe ya bahari ya Indi.

No comments