BABA AJINYONGA NDANI YA NYUMBA YA MWANAE TARIME
>> Mjumbe ashangazwa matukio ya kujinyonga mtaani kwake Kogete
Na Helena Magabe , Tarime
Mwanaume mmoja aitwaye John Muhabe maarufu John Msabato mkazi wa mtaa wa Kogete, wilaya ya Tarime, mkoani Mara, amekutwa amejinyonga ndani ya nyumba ya kijana wake hadi kufa
Mwili huo umekutwa ndani ya nyumba jana asubuhi Januari 30, 2025 , inasemekana tukio hilo alilifanya usiku wa Januari 29, 2025 nyumbani mtaa wa Kogete kata ya Kenyamanyori.
Mjumbe wa serikali ya Mtaa wa Kogete Frola Joel ambaye ni shuhuda wa tukio hilo amesema amefika na kukuta mwili wa Marehemu ukiwa umening'inia kwenye chumba alichojinyongea huku mahindi yakiwa yametandazwa chini.
" Mimi nimeshuhudia nimekuta mwili bado umening'inia marehemu akiwa amevaa nguo zake na viatu , mahindi yakikuwa yametandazwa chini , alifunga kamba ndefu mpya kabisa.
" Polisi wamekuja kuchukua mwili na kuondoka nao. Nasikitika sana na matukio haya yakujinyonga mtaani kwetu mwaka jana mwezi watu walijinyonga watu wawili mama jirani na kijana sijui nini kimetokea mtaani" amesema Frola.
Mke wa Marehemu John Muhabe, Rebeca John Muhabe amesema marehemu mumewe alikuwa akilala kwenye nyumba ya kijana wake ambaye haishi Tarime na alikuwa akilala kwenye nyumba hiyo kwa lengo la kulinda mahindi yasiibiwe waliyokuwa wameyavuba nakuyahifadhi katika nyumba hiyo .
Amesema jana usiku marehemu alipewa chakula akala akiwa kawaida bila kuonyesha hali yoyote, alikula kiasi akaenda kulala na mjukuu wake ambaye amekuwa akilala naye kwenye chumba hicho.
" Asubuhi niliamka kukinga maji ya mvua iliyokuwa ikinyesha lakini nikasikia mjukuu anamuita babu yake, nikachungulia na kumkuta mume wangu kajinyonga.
" Kumbe alikuwa amenunua kamba sijui hata alikuwa ameificha wapi, hatukuwa na ugonvi wowote,nilisikia mjukuu akimuita sokoro sokoro (,Babu babu) nikamwuliza sokoro hayumo ndani akasema hayumo ndio nikachungulia kumbe alikuwa amejinyonga" amesema Rebeca.
kijana wa nne katika familia hiyo Samwel John Muhabe amesema anasikitishwa na kitendo alichokifanya marehemu baba yake kwani waliishi naye vizuri bila shida yoyote na hakuwahi kuwashirikisha kama kuna changamoto yoyote anaipitia.
Amesema baba yao alinunua kamba mpya kwani hakukuwa na kamba yoyote hapo nyumbani kwao, hivyo wanasikitika wao kama Familia kwa kitendo hicho ambacho baba yao amekitenda kwani inaonyesha alijiandaa kujiua.
Majirani wamesikitishwa na hatua hiyo aliyoichukua marehemu, wamesema alikuwa mkimya ambaye hakuwa na matatizo na majirani zake.
Baadhi waliomuona siku chake kabla ya kifo chake wamesema alikuwa amepungua lakini bado alikuwa mwenye uchangamfu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Polisi, Tarime/ Rorya RPC Mack Njera hakuweza kupatikana kwenye simu yake ili kuthibitisha juu ya tukio hilo.
Simu yake haikupokelewa baada ya kupigiwa simu zaidi ya mara moja bila kupokelewa. Mwili huo umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hosiptali ya wilaya ya Tarime (Bomani ).
Post a Comment