HEADER AD

HEADER AD

BILIONEA MAARUFU DUNIANI AGA KHAN AMEFARIKI AKIWA NA UMRI WA MIAKA 88


BILIONEA maarufu  duniani na kiongozi wa kiroho wa dhehebu la Ismaili katika dini ya Kiislamu, Aga Khan, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88.

Kifo chake kimetangazwa siku ya Jumatano na Wakfu wa Aga Khan Developtment Network, ambao umesema alifariki dunia kwa amani jijini Lisbon nchini  Ureno, akiwa amezungukwa na familia yake.
          Bilionea maarufu  duniani na kiongozi wa kiroho wa dhehebu la Ismaili katika dini ya Kiislamu, Aga Khan, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88. REUTERS - Mark Blinch.

Mzaliwa huyo wa Sweden, aliyekuwa na uraia wa Uingereza na Ureno, alianzisha miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo hospitali na shule kwa lengo la kuwasaidia, watu wa kawaida, katika nchi za afrika na bara Asia.

Alikuwa ameekeza katika shule na hospitali nchini Kenya.
Alikuwa ameekeza katika shule na hospitali nchini Kenya. AFP - YASUYOSHI CHIBA

Aga Khan wa nne, ambaye jina lake halisi ni Mwanamfalme Karim Al-Hussaini, ameombolezwa na viongozi mbalimbali kama mfanyabiashara na tajiri aliyegusa maisha ya watu.

Maisha yake ya utotoni aliishi nchini Kenya na baadaye akaenda Tanzania kuendeleza biashara za babu yake mwaka 1957 katika nchi hizi mbili, alizowekeza pakubwa.

Rais wa Kenya William Ruto na Suluhu Hassan wa Tanzania, wameomboleza kifo chake na kumsifia kwa mchango na uwekezaji wake mkubwa katika sekta ya elimu na afya katika nchi zao.

Naye, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amemwelezea Aga Khan kama nembo ya amani, aliyehubiri mshikamo na kukariri kuwa dini ya Kiislamu.

Chanzo : RFI

No comments