HEADER AD

HEADER AD

MGORE : UCHUMI WA MARA UTAONGEZEKA ENDAPO WATU WATAWEKEZA KWA WINGI

>>Sokombi asema Mara ina fursa nyingi za uwekezaji

Na Jovina Massano, Musoma

IMEELEZWA kuwa, uchumi wa mkoa wa Mara utaongezeka ikiwa wawekezaji watawekeza kwa wingi katika sekta ya utalii, bandari, viwanda.

Pia ukamilikaji wa uwanja wa ndege wa Musoma utachochea ongezeko la  wageni wengi na hivyo kukuza uchumi katika mkoa huo .

Hayo yamesemwa na mjumbe Baraza kuu wazazi Taifa wa chama cha Mapinduzi Mgore Miraji Kigera  hivi karibuni wakati wa ziara ya uimarishaji chama ya makamu mwenyekiti wa CCM Taifa Steven Masatu Wasira  mkoani hapa.

      Mjumbe Baraza kuu wazazi Taifa wa chama cha Mapinduzi Mgore Miraji Kigera

Akiongea na DIMA ONLINE Mgore amesema hivi sasa mkoa una mabadiliko ya kimaendeleo , lakini ili kuendana na kasi hiyo, mkoa unahitaji uwepo wa uwekezaji mkubwa ili kuwasaidia wananchi katika kukuza vipato vyao na ukuaji wa uchumi na kuweza kuzihudumia familia zao kwa usahihi.

Amesema uboreshaji huduma za kijamii katika mkoa huo unaendelea  kufanywa na serikali ikiwemo ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan umewezesha mazingira rafiki kwa wawekezaji kuja kuwekeza.

"Miundombinu inazidi kuimarika nchi kavu, anga na majini, tunashuhudia ongezeko la vituo vya afya, miundombinu safi ya elimu, nishati sambamba na upatikanaji wa maji Safi na salama" amesema.

Ameongeza kuwa, ongezeko la wawekezaji litachangia kupaisha uchumi wa mkoa hivyo wananchi wenye uwezo wa kuwekeza wachangamkie fursa kwa kuwekeza katika maeneo mbalimbali.  

"Makamu Mwenyekiti wetu amesema wazi kabisa kuwa wananchi wanahitaji uchumi na maisha bora hivyo kurudisha huduma za bandari kutaongeza kasi ya maendeleo ya mkoa na tunaendelea kufurahia matunda ya chama cha Mapinduzi".

Mgore hakusita kuipongeza kamati kuu ya Taifa ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM ambae ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na kuipa heshima kubwa mkoa wa Mara, kumteua makamu Mwenyekiti wa CCM kutoka mkoa.

Mfanyabiashara Joyce Bitta Sokombi amesema mkoa una fursa nyingi za uwekezaji ni mji wa utalii  ikiwemo mbuga na makumbusho ya kihistoria ya Baba wa Taifa ).

      Mfanyabiashara Joyce Bitta Sokombi

"Mkoa una madini na ziwa lenye rasilimali nyingi zikiwemo samaki na dagaa. Serikali ya awamu ya sita ni jibu pia ni maji ukiwa na kiu na sauti ya wasio kuwa na sauti katika jamii yetu, sisi wananchi wa Mara tunawakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ili kuwasaidia kukuza uchumi wetu.

"Amani, utulivu tulionao hapa nchini ni uimara wa viongozi waadilifu unaonyesha na kuwezesha uwepo wa mazingira rafiki kwa kuwekeza popote nchini usalama tulionao ni tunda imara kwa Taifa."amesema Sokombi.

Ameongeza kusema " Hii ni serikali yenye nia njema na ustawi wa Taifa lake, inaendelea kuleta mabadiliko ya maendeleo kwa wananchi wake, viongozi wanaoshikamana wanaotumikia wananchi kwa usawa, mwenye macho haambiwi tazama" amesema Sokombi.

               

No comments