DAKTARI ZAHANATI YA KIBAGA HANA CHOO AJISAIDIA CHOO CHA WAGONJWA
Na Helena Magabe , Tarime
DAKTARI anayetoa huduma ya afya katika Zahanati ya Kibaga Kata ya Kenyamanyori, wilaya ya Tarime mkoani Mara jina linahifadhiwa, anajisaidia katika choo cha wagonjwa kwakuwa nyumba anayoishi ya serikali haina choo.
Akizungumza na DIMA ONLINE, Mwenyekiti wa mtaa wa Kibaga , Erasto Dismas amesema Zahati hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa choo katika nyumba ya mganga na Zahanati kukosa umeme.
"Nyumba ya mganga imejengwa na serikali, ni nzuri lakini haina choo, mganga analazimika kwenda kujisaidia kwenye choo cha Zahanati. Tunaomba serikali itengeneze mazingira mazuri kwa watoa huduma wetu ili wawe na moyo wa kufanya kazi wasiweze kukata tamaa kutokana na mazingira magumu ya kazi" amesema Mwenyekiti wa mtaa .
" Tunaiomba Serikali ijenge choo cha mganga na Zahanati iwe na umeme. Vipimo vinakwama kufanyika kwa sababu hakuna umeme. Pia kuna dawa zinatakiwa kuhifadhiwa kwenye friji (Jokofu) lakini kutokana na ukosefu wa umeme dawa hizo zinakosekana katika Zahanati.
Diwani wa Kata ya Kenyamori Farida Joel akizungumza kwa njia ya simu akiwa safarini Jijini Dodoma, amesema Zahanati hiyo ina mganga mmoja na nyumba moja ya mganga isiyo na choo na Zahanati haina umeme.
"Pale kwenye Zahanati pana changamoto ya ukosefu wa choo kwenye nyumba ya mganga, anatumia choo cha wagonjwa cha Zahanati.
"Zahanati haina umeme , usiku anatoka kwake anaenda Zahati na ukizingatia sio mzawa wa Tarime usalama wake unaweza kuwa mdogo. Nimeomba umeme siku nyingi na choo kijengwe lakini bado" Amesema Farida.
Katika kikao cha Baraza la Madiwani halmashauri ya mji Tarime, kilichoketi Januari , 4, 2025 , Mwenyekiti wa halmashauri hiyo , Daniel Komote akagusia changamoto ya ukosefu wa umeme Zahanati ya Kibaga. Ameliomba Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) kupeleka umeme katika Zahanati hiyo.
Amesema ukosefu wa umeme umechangia kutofanyika baadhi ya vipimo licha ya huwepo wa dawa hivyo ni vyema TANESCO ikaharakisha kupeleka umeme ili wagonjwa wapate huduma ya vipimo.
Kaimu Meneja TANESCO Frednand Mhushi amesema wametenga nguzo 10 za kupeleka kwenye zahanati hiyo, nguzo tano kwaajili ya zahanati na nyingine kwa majirani walio karibu na zahanati na amesema nguzo hizo zitapelekwa ndani ya mwezi huu wa Februari.
Post a Comment