HEADER AD

HEADER AD

MAHAKAMA KUU KANDA YA BUKOBA YAITUNUKU DIMA ONLINE CHETI CHA SHUKRANI

Na Mwandishi wetu, Bukoba

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Bukoba, imetoa cheti cha shukrani kwa chombo cha habari cha mtandaoni DIMA ONLINE ikiwa ni kutambua ushiriki mzuri katika kuhabarisha na kuelimisha jamii masuala mbalimbali ya kisheria katika wiki ya sheria nchini.

Cheti hicho kimekabidhiwa kwa Mwandishi wa habari wa DIMA ONLINE Alodia Dominick , wakati wa kilele cha siku ya sheria nchini , Februari 03, 2025 ambapo mwandishi huyo aliripoti habari mbalimbali za kuelimisha jamii katika wiki ya sheria katika chombo hicho cha habari.

   
         Mwandishi wa DIMA Online Alodia Dominick akipokea  cheti cha shukrani cha DIMA ONLINE toka kwa Jaji mfawidhi mahakama kuu kanda ya Bukoba Immaculata Banzi  (kushoto) pamoja na kaimu mkuu wa mkoa wa Kagera ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Sima ( wa pili kulia).

Wanasheria katika mkoa huo walitoa mada mbalimbali katika wiki ya sheria inayoadhimishwa Januari 25 hadi Februari, 01 kila mwaka ambapo walitoa elimu ya sheria zikiwemo sababu za ukatili wa kijinsia, migogoro na ndoa.

Mwandishi huyo amepokea cheti kutoka kwa aliyekuwa mgeni rasmi katika wiki ya sheria mkoani Kagera, Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Bukoba, Immaculata Banzi katika kilele cha wiki ya sheria na siku ya kuashiria kuanza shughuli za mahakama mwaka huu.

"Tunashukuru DIMA ONLINE kupitia Mwandishi wake Alodia Dominick kwa kujitoa kwa moyo wa dhati kuelimisha jamii kupitia habari zetu alizoziandika na kuchapishwa katika chombo hiki cha habari.

" Tunashukuru pi na vyombo vingine vya habari vilivyopo  Kagera na nje ya Kagera ambavyo ni  radio, Television, TV , Mitandao ya kijamii pamoja na magazeti  kwa kazi nzuri ya kujitoa kwa moyo safi katika wiki ya sheria na kuelimisha umma wa watanzania" amesema Jaji Immaculata.

Amesema kuwa, katika wiki ya sheria mahakama kuu  kanda Bukoba wameweza kutoa elimu katika sehemu mbalimbali yakiwemo magereza yote yaliyopo mkoani Kagera, wafanya biashara, katika mialo ya wavuvi, sokoni, waendesha pikipiki, vyuoni pamoja na shuleni.

Naibu msajili mahakama kuu kanda ya Bukoba, Said Mkasiwa amesema, wiki ya sheria inawawezesha wananchi kupata elimu ya masuala mbalimbali ya kisheria na inaashiria kuanza rasmi mwaka wa mahakama.

Mwandishi wa habari wa Alodia Dominick ameipongeza mahakama hiyo kwa kutambua mchango wake katika kuhabarisha jamii wiki ya sheria kupitia chombo hicho cha habari.

           Cheti cha shukrani kilichotolewa na Mahakama kuu kanda ya Bukoba

"Naishukuru  Mahakama kuu kanda ya Bukoba kwa kuitunuku DIMA ONLINE cheti kupitia mimi mwandishi wa chombo hicho cha habari mkoani Kagera. Tutaendelea kushirikiana na mahakama katika shughuli mbalimbali za kuelimisha jamii" amesema Alodia .

Mkurugenzi mtendaji wa DIMA ONLINE, Rose Kimaro, ameishukuru Mahakama kuu kanda ya Bukoba kwa kukitunuku cheti chombo hicho cha habari na kusema kuwa imeiheshimisha DIMA Online.

" Sisi kama uongozi wa DIMA Online tunaishukuru sana Mahakama kuu kanda ya Bukoba kwa kukipatia cheti cha shukrani chombo chetu cha habari. Tunaihidi kuendelea kuhabarisha umma katika nyanja mbalimbali zikiwezo habari za mahakama na zinginezo" amesema Rose.

Mkurugenzi huyo amempongeza mwandishi wa habari wa chombo hicho Alodia Dominick kwa kujituma katika kuripoti habari mbalimbali katika mkoa huo , na kwamba juhudi hizo ndio matokeo ya kupata cheti cha shukrani katika kuhabarisha wananchi.

       
       Mkurugenzi mtendaji wa DIMA ONLINE, Rose Kimaro

" Nampongeza Alodia kwa kazi nzuri kwani endapo asingejitoa kwa bidii katika kuhabarisha jamii sidhani kama mahakama ingetutunuku cheti.

" Imefanya hivyo kwasababu imetambua mchango wa Alodia kupitia DIMA ONLINE kuhabarisha wananchi katika masuala mbalimbali ya kisheria yaliyotolewa na wanasheria wakati wa maadhimisho ya wiki ya sheria" amesema Rose.

Kauli mbinu ya wiki na siku ya sheria mwaka huu inasema " Tanzania 2050 : Nafasi ya Taasisi zinazosimamia Haki madai katika kufikia malengo makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo" .

Maadhimisho ya wiki ya sheria na siku ya sheria nchini hufanyika kila mwaka kuashiria mwanzo wa kuanza kwa shughuli za mahakama kwa mwaka husika baada ya kumalizika kwa likizo ya mahakama inayoanza kila tarehe 15 Desemba na kumalizika tarehe 31 Januari ya mwaka unaofuata.

Maadhimisho ya wiki ya sheria ni sehemu muhimu ya jitihada za kuimarisha utawala wa kisheria nchini Tanzania , na ushiriki wa Tume ya Kurekebisha sheria unaonesha dhamira yake ya kuhakikisha sheria zinaendena na mahitaji ya jamii.


No comments