DEO MECK ACHANGIA MATOFALI UJENZI SHULE MPYA KOGETE
Mwenyekiti asimulia umbali wa shule ulivyomkatili mwanae
-Diwani asema ujenzi wa shule utapunguza ukatili
Pesa za mfuko wa kamati ya maafa zatumika kujenga shule
Na Helena Magabe, Tarime
WANANCHI wa Mtaa wa Kogete ,kata ya Kenyamanyori , wilaya ya Tarime mkoani Mara, wamelazimika kuanza ujenzi wa shule mpya ya msingi ili kuwaepusha watoto kutendewa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mwenyekiti wa mtaa wa Kogete Aliphaxad James, kwa kushirikiana na Diwani wa kata ya Kenyamanyori Farida Joel na wananchi wameanza ujenzi wa vyumba viwili kwa nguvu za wananchi kupitia mfuko wa maafa ambapo zaidi ya Tsh. Milioni 1.5 zimetumika na ujenzi huo unaendelea.
Hatua hiyo ya ujenzi wa shule imekuja baada ya watoto kuwa kwenye hatari ya kufanyiwa ukatili wakati wakienda au kutoka shule jirani mtaa wa Tagota.
Kutokana na changamoto ya ukatili wa kijinsia kwa watoto, mdau wa maendeleo, Deogratius Meck amekuwa wa kwanza kuunga juhudi za wananchi kwa kuchangia matofali 300 zenye thamani ya Tsh. 420,000 baada ya kuombwa msaada na Diwani wa Kata hiyo na mwenyekiti wa mtaa huo.
Akiwasilisha mchango kwa niaba ya mdau huyo, Pasco Maswi amekabidhi matofali hayo Februari 13,2025, asema lengo ni watoto wapate elimu, wajekuwa viongozi mbalimbali Nchini.
Pasco Maswi (katikati) akizungumza jambo wakati alupokabidhi tofari 300 ujenzi wa shule mpya ya msingi Kogete, kushoto ni Diwani Kata ya Kenyamanyori, na Mwenyekiti wa mtaa wa Kogete Aliphaxad James.
Amesema kuwa, Deogratus ni mtu wa kujitoa kusaidia na hatakomea hapo endapo atapewa ushirikiano, na kuongeza kuwa wakipatikana watoro wa mazingira magumu atawasaidia kwani hivi karibuni alichangia watoto wa mazingira magumu mahitaji ya shule.
Amewaomba viongozi hao kushirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo bila kujali itikadi zao ili kuhakikisha shule inakamilika haraka na watoto waanze kusoma.
"Deo Meck alisomeshwa na wazazi wake kwa mazingira magumu anataka watoto wasome wapate nafasi wawe kama viongozi wengine waliowahi kuwa wabunge kutoka Tarime kama Kembaki,Heche, wawe kama Diwani Farida, wengine waje kuwa Maraisi, makamu wa Rais au mawaziri "amesema Maswi.
Ukatili aliofanyiwa mtoto wa Mwenyekiti
Mwenyekiti wa mtaa wa Kogete ni Mhanga wa ukatili wa kijinsia kupitia Binti yake jina limehifadhiwa aliyefanyiwa ukatili wa kijinsia na watu wasiojulikana akiwa njiani kuelekea shuleni iliyopo umbali mrefu.
Amesema tukio hilo limewemeka kovu moyoni mwake na kuwa funzo kwake na hivyo kuhamasisha ujenzi kuanza haraka kwa kushirikiana na wananchi pamoja na Diwani.
" Sitosahau tukio la ukatili aliofanyiwa binti yangu Octoba,10,2024 alipovamiwa njiani akielekea shuleni na kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana, jambo lililonipelekea kuona kuwa kuna haja ya watoto wakike kuhakikishiwa usalama wao kwa kusoma mazingira ya karibu vilevile kupunguzia watoto mwendo wa kusoma mbali.
Diwani wa kata ya Kenyamanyori Farida Joel amesema anachukizwa na ukatili wa kijinsia unavyofanyika kwenye kata yake na kwamba umbali wa shule ndio chanzo cha kufanyika kwa ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike kwenye kata hiyo.
" Hali hiyo ilipelekea tufanye jitihada za kupata eneo la kujenga shule ili kupunguza ukatili kwa kuhakikisha watoto hawatembei umbali mrefu kwenda shuleni. Watoto wa darasa la kwanza wanapokuwa watoka shule ya msingi Tagota wakati mwingine wanabakwa.
" Vilevile shule hiyo kwa sasa imejaa ina wanafunzi wengi ndio maana tumeona tuanzishe shule mpya kwa kutumia mfuko wa kamati ya maafa ili kuwapunguzia wazazi mzingo wa michango.
"Tunawaomba na wadau wengine wa maendeleo watuunge mkono ili kufanikisha ujenziwataendelea kuwaomba wadau mbalimbali ili kufanikisha ujenzi " amesema Diwani Farida.
Mkazi wa mtaa wa Kogete Mgendi Kebagiri Mwita amewashukuru viongozi hao kumtafuta mdau ambaye ameweza kuchangia matofali 300 zitakazo songeza ujenzi wa shule hiyo.
Post a Comment