Home
/
MICHEZO/BURUDANI
/
IRENE ISHENGOMA AUPONGEZA MTANDAO WA WANAWAKE KUIBUA VIPAJI SOKA LA WANAWAKE TEMEKE
IRENE ISHENGOMA AUPONGEZA MTANDAO WA WANAWAKE KUIBUA VIPAJI SOKA LA WANAWAKE TEMEKE
Na Andrew Chale, Temeke
MJUMBE wa Kamati Tendaji ya Chama Cha Mpira wa miguu kwa wanawake Tanzania (TWFA) ambaye pia ni mdau wa michezo nchini, Irene Ishengoma, ameupongeza mtandao wa wanawake laki moja kwa kuwezesha kufanyika ligi ya soka kwa wanawake ndani ya Temeke iliyopewa jina la Wanawake Laki Moja Cup 2025.
"Najivunia sana kiongozi mlezi wa Wanawake Laki Moja, Mama Tano Mwera, Dada Mwanaharusi Kingwendu Mratibu wa mashindano haya, Viongozi wa mpira wa miguu kwa Wanawake Temeke (TEWFA)Bw. Yasin Nonji na wengine wote hakika wamefanya jambo kubwa na la kihistoria kwa mabinti hawa.
" Nipongeze TFF, TWFA, kwa kuendelea kusongesha mbele gurudumu la maendeleo ya soka la wanawake Tanzania ndio maana wadau wanazidi kujitokeza na kufanya mambo makubwa ikiwemo kudhamini mashindano kama walivyofanya wanawake Laki Moja." Amesema Irene Ishengoma.
Aidha, Irene amewataka wadau wa soka la wanawake kuendelea kuunga mkono michezo hiyo ikiwemo kuwashika mkono ilikuendelea kuibuka vipaji vingi kwani soka ni ajira kwa sasa na Tanzania imekua moja ya nchi zinazoendelea kufanya vyema katika soka hilo kwa Wanawake.
Mlezi wa Mtandao huo wa Wanawake Laki Moja Tano Mwera na mdhamini wa Ligi hiyo ya Wanawake Laki Moja Cup 2025, amewapongeza waratibu wa mashindano hayo na kuwaahidi kuendelea kuwashika mkono katika jambo la michezo kwani Soka ni ajira.
"Tunashukuru kwa kumaliza salama jambo letu tumehitimisha leo. Hongera wote walioshiriki na walioshinda, niwapongeze Temeke Sisters kwa ushindi wenu . Asanteni kwa timu zote shiriki na wadau wote mlioshiriki kwa njia moja au nyingine nawapenda sana " amesema Tano.
Mtandao wa wanawake Laki moja milango ipo wazi kwa wadau na waratibu wa soka la Wanawake karibuni tupo tayari kushirikiana". Amesema Mhe DC Mstaafu Tano Mwera.
Aidha, katika fainali hiyo, Timu ya Temeke Sisters iliweza kuibuka mabingwa kwa ushindi wa bao tatu kwa mbili dhidi ya Sayari Women.
Mshindi wa kwanza aliweza kukabidhiwa Tsh 500,000 taslimu, huku wa pili akipata Tsh 300,000 na kwa mshindi wa tatu amepata Tsh 200,000 na nne alipata Tsh. 150,000.
Post a Comment