JESHI LA POLISI TARIME RORYA LATHIBITISHA KUKAMATWA MWENYEKITI WA CCM
>> Laanza uchunguzi
Na Mwandishi Wetu, Tarime
JESHI la Polisi mkoa wa Polisi Tarime Rorya limekiri kupokea taarifa ya kukamatwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Itiryo na wengine wawili, wote wakazi wa Kijiji cha Itiryo , Kata ya Itiryo wilaya ya Tarime mkoani Mara.
Jeshi hilo limethibitisha tukio hilo kupitia akaunti ya Polisi Tarime Rorya katika mtandao wa Instagram, taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tarime , Rorya, leo Februari, 12, 2025.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Jeshi la Polisi limepokea taarifa ya kukamatwa kwa watu watatu wakazi wa Kijiji cha Itiryo, wilaya ya Polisi Nyamwaga wamekamatwa na watu ambao hawajafahamika .
Jeshi hilo limewataja waliokamatwa ni Muriba Mugahu Muhere , (41), Dereva na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Itiryo, Lucus Mwera Chacha maarufu Kamanda (71) na Mwita Gesabo (45).
Taarifa za awali zilizoripotiwa Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa mnamo 9/02/2025 majira ya saa saba usiku katika Kijiji cha Itiryo, watu watano wakiwa na silaha za moto waliruka ukuta wa nyumba ya Muriba Mugahu Muhere kisha kumkamata .
Aidha, watu hao walifika kwa Lucus Mwera Chacha na Mwita Ghati Gesabo kuwakamata na kuondoka nao.
Jeshi la Polisi baada ya kupokea taarifa limeanza uchunguzi ili kubaini wahusika wa matukio hayo baada ya uchunguzi huo kukamilika litatoa taarifa kamili.
Jeshi la Polisi Tarime Rorya limetoa wito kwa mwananchi yeyote mwenye taarifa inayoweza kusaidia uchunguzi anakaribishwa.
>> Rejea
Siku moja iliyopita chombo hiki cha habari kiliripoti habari yenye kichwa cha habari ' RPC TARIME RORYA NA UKIMYA KUTEKWA MWENYEKITI WA CCM'
Post a Comment