HEADER AD

HEADER AD

TRA : UTOAJI RISITI ZISIZO ZA KIELETRONIKI UNAISABABISHIA HASARA SERIKALI

Na Jovina Massano, Musoma

UTOAJI risiti zisizo sahihi za kieletroniki ( EFD), bidhaa za magendo zikiwemo bidhaa zenye stempu za kugushi zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiashara kukosesha takwimu sahihi za biashara na kuisababishia serikali serikali kupata hasara.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na naibu Kamishna wa uwezeshaji biashara wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wahabi Matengo wakati  wa sherehe ya utoaji tuzo ya siku ya mlipakodi zilizotolewa na mamlaka hiyo iliofanyika katika ukumbi wa MK uliopo Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma mkoani Mara.


Wahabi amesema pamoja na kwamba mamlaka inatambua mchango uliofanywa na walipa Kodi bado kuna changamoto za baadhi ya wafanyabiashara kutotumia mashine za kutolea risiti kwani matumizi sahihi ya mashine hizi ndio msingi mkuu wa kupata takwimu sahihi  za biashara na kuwezesha ukadiliaji wa ukusanyaji wa kodi sahihi na kuondoa malalamiko kwa wateja.
  
"Nitoe rai kwa wafanyabiashara kuacha tabia hiyo na wale wauzaji wa bidhaa na vinywaji zinazobandikwa stempu hakiki uhalali kwa kutumia mfumo wa hakiki stempu kwa kutumia App katika simujanja kwa kupakua.

"Wale wanaoingiza mizigo kwa njia ya magendo kuacha kwani bidhaa nyingi zinakuwa hazijahakikiwa na mamlaka za uthibiti na viwango," amesema Wahabi.

Amesema katika kuhakikisha mafanikio ya kiutendaji ndani ya mamlaka yanaimarika na kuwa endelevu kwa sasa mamlaka inaendelea na mpango mkakati wake wa sita ulioanzishwa mwaka 2022/2023.


Pia imejiwekea malengo ambayo yanawawezesha uhiari, imani na ridhaa kwa walipakodi kwa kuendelea kuboresha mifumo na kuioanisha na hii inaendana na mipango mikakati ya Taifa.

Uwezeshaji wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuioanisha mifumo utasaidia kupunguza ghalama na adha kwa walipakodi na utaongeza ukusanyaji wa Kodi.

Hata hivyo meneja wa mamlaka hiyo mkoani hapa Nasoro Ndemo amesema mamlaka imekuwa ikiwapa ujuzi watumishi wake sambamba na utoaji elimu kwa walipakodi lengo ni kuwezesha ulipaji Kodi wa hiari na kuleta ongeko la mapato katika mkoa.

     Meneja wa mamlaka hiyo mkoani hapa Nasoro Ndemo

"Kuna  changamoto ambazo zinakwamisha katika ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa baadhi ya wafanyabiashara kushindwa kuwasilisha ritani zao kwa wakati na kulipa Kodi kwa wakati lakini pia wapo baadhi wanaokwepa kusajili biashara zao,"amesema Nasoro.

Hakusita kuelezea mafanikio yaliyosababisha ukuaji wa mapato mkoani hapa ambapo pato la robo ya mwaka Julai hadi Desemba 2024  limefikia asilimia 104 ya lengo hii imechangiwa na mazingira mazuri ya biashara na ushirikiano mzuri kwa walipakodi wanaotimiza wajibu wao na kulipa Kodi kwa wakati na uwepo wa mifumo thabiti uliowekwa na serikali ya awamu ya sita.

Meneja wa kampuni ya Singita Trading Stores inayojihusisha na uuzaji wa bidhaa kwa wageni wa kitalii wanaokuja mbugani Wilayani Serengeti, Moses Malinga Kagaruki ambae pia ameiwakilisha Grumet Construction Limited amesema kuwa ukwepaji wa kodi ni kurudisha maendeleo ya Taifa nyuma na ulipaji wa Kodi ni kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Ameipongeza mamlaka ya mapato kwa utoaji tuzo kwa walipakodi kwani hii inaongeza hamasa kwa walipakodi na kuwa na ukaribu na wateja.

"Ombi letu kwa wizara husika kuhakikisha wanauboresha mfumo ili wakati wa malipo kusiwe na changamoto wakati wa kutuma ritani kwa wakati,mara nyingi muda ukifika wa kutuma VAT mfumo una shida ya mtandao inafikia hatua tunatafuta msaada kwa maafisa wa mamlaka na wao hutusaidia na kutuongezea muda wa malipo," amesema Moses.

Mtendaji wa Chemba ya biashara ,viwanda kilimo na uvuvi (TCCIA) Fransis Ngowi amesema juhudi kubwa zilizofanywa na Taasisi hiyo ni kusogeza huduma rafiki za TRA kwa wafanyabiashara.

Amefafanua kuwa TCCIA ni chombo kilichoundwa kwa sheria ya bunge mwaka 1988 lengo kuu la taasisi ni kusimamia sekta binafsi nchi nzima na ndio msemaji mkuu wa sekta binafsi kwa serikali.

" Tumeshuhudia mabadiliko mengi yanayofanywa na serikali baada ya ushauri na ushawishi wa TCCIA kwa serikali hakuna ambae hakumbuki miaka ya nyuma maafisa  wa mamlaka ya mapato walikuwa wakipita na makufuli wakifunga maduka huku baadhi ya watu walikuwa wakifunga maduka kwa kuwakimbia jambo hili tumeshuhudia wote", amesema Ngowi .

Ameongeza kusema " Ameongeza kuwa kwa juhudi kubwa ya Taasisi yetu imeweza kuishawishi serikali  kuchukua hatua kubwa kusogeza huduma za TRA kuwa rafiki kwa wafanyabiashara na kuipongeza serikali ya awamu ya sita kwa Ujenzi mkubwa wa  maboresho ya mazingira ya biashara.

" Katika mkutano mkuu wa  TCCIA Disemba 6, 2024 Taasisi imesaini mkataba wa mashirikiano na TRA ikiwa na lengo la kuongeza idadi ya walipakodi kwani ongezeko hilo  litasaidia kupunguza ghalama za Kodi na kuleta unafuu kwa wanaolipa mapato" amesema .

Mgeni rasmi katika sherehe hizo kwa niaba ya mkuu wa mkoa Kanali Evans Mtambi , mkuu wa wilaya ya Musoma Juma Chikoka amesisitiza utoaji wa elimu kwa walipakodi na wananchi wote ili kuwezesha maendeleo ya Taifa kwa kuwa serikali inathamini walipakodi kwa kuwa upatikanaji wa huduma za kijamii zikiwemo ajira ni matokeo ya kodi hizo.

Wakati huohuo, Katika sherehe hizo mamlaka ya mapato mkoani hapa wameweza kutoa vyeti kwa walipakodi wasikwepa kulipa Kodi, wanaolipa kodi kwa wakati walipaji wa kati  sambamba na kuwatunuku tuzo Taasisi za umma kwa kusaidia ukusanyaji wa mapato.

Wanaosaidia mamlaka ya Mapato katika ukusanyaji wa mapato ni Mkuu  wa mkoa wa Mara,Afisa Madini Mkoa( RMO ) na Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalum Rorya na Tarime.

Idara ya walipakodi wa kati walioko mkoani hapa ambao ni Grumet Construction Limited,Farai Logistics Co.Limited na Zem(T) Co.Limited.

Ukanda wa Sirari, Joseph Nyabaturi Makore, Elizabeth Benard Njeri na Muhono Samwel Mwita huku Nyamongo wakiwemo W&H Geney Supply&co.Limited,GM Technosolution Ltd na Lacuna Co.Ltd

Wilayani Butiama wametunukiwa Julius Marwa Warioba, Samwel Simburya Mgendi na Ressurection Pre& Primary School. Wilaya ya Rorya ni Ongujo Investment Ltd, Charles Ochele Obuto na Maji Safi group.

Kutoka Wilayani Serengeti waliopata tuzo ni SH Lodge Ltd,Singita Trading Stores (East Africa)Ltd , Grumeti huku Wilaya ya Bunda waliopewa ni Bunda Logistics Co.Ltd, Robert Chacha Maboto na Safari Suites Ltd.

Tarime mjini ni Batholomeo Mwikwabe Machage, Agnes Mwita Chacha na Bisma Traders na Wilaya ya Musoma wakiwemo Mehboob Imitiaz Agency na Chacha Marwa Wambura.

Walipakodi wa forodha ni Sandvic Mining& construction.Ltd ambae pia amepata tuzo za ulipaji kodi kwa wakati na asiekwepa kulipa Kodi,Mantrac Tz Ltd na North Mara Gold Mine lakini pia mawakala wa forodha hawakusahaulika katika tuzo hizo ambapo Freight Forwarders TZ Ltd, African Global Logistics na Trans pack TZ Ltd ni miongoni mwa waliotunukiwa tuzo na mamlaka hiyo.
       Meneja wa Kampuni ya Singita Trading Stores (East Africa) Ltd Moses Malinga Kagaruki.




No comments