MADAKTARI BINGWA HOSPTALI YA RUFAA MARA WATUA TARIME KUHUDUMIA WANANCHI
> >Ni madaktari bingwa wa wanawake, watoto, mifupa, kinywa, pua na masikio, macho, uzazi, magonjwa ya ndani
>> Zaidi ya wananchi 800 wajitokeza kupata huduma.
>> Mganga Mfawidhi hospitali ya wilaya ya Tarime awaomba wananchi waendelee kujitokeza
MGANGA Mfawidhi hospitali ya wilaya ya Tarime ,mkoa wa Mara Yonam Charles amewaomba wananchi kuendelea kujitokeza katika hospitali hiyo ili kupata huduma ya vipimo na matibabu kutoka kwa madaktari bingwa wapatao saba waliofika Tarime kutoa huduma ya kibingwa.
Madaktari hao wametoka hospitali ya Rufaa ya mwalimu Nyerere mkoani Mara, ambao wameanza kutoa huduma ya kibingwa kuanzia februari , 24,2025 na watahitimisha huduma Machi, 01,2025.
Akizungumza na Waandishi wa habari wa DIMA Online , Februari, 27, 2025, Mganga Mfawidhi amesema hospitali imepokea madaktari bingwa wa macho,upasuaji wa pia,kinywa masikio, magonjwa ya ndani, upasuaji wa mifupa, magonjwa ya wanawake , dakrati bingwa wa watoto na wanawake.
Amesema hadi kufikia jana ,wagonjwa zaidi ya 800 wenye matatizo mbalimbali wamejitokeza katika Hosptali ya wilaya ya Tarime kwajili ya kuonana na kupatiwa matibabu na madaktari bingwa 7 na kupata matibabu kwa gharama nafuu.
Dkt.Yonam amesema mwitikio ni mkubwa kwani ndani ya siku tatu tangu februari 24 hadi 26 wagongwa 820 wamejitokeza kuonana na madaktari bingwa wapatao saba na kupata huduma.
Wagonjwa wakiwa kwenye foleni hospitali ya wilaya ya Tarime wakisubiri huduma kutoka kwa madaktari Bingwa hospitali ya rufaa ya mwalimu Nyerere mkoa wa Mara
"Mwitikio wa wananchi kujitokeza ni mzuri , wagonjwa waendelee kujitokeza wasisubirie siku ya mwisho. lengo ni kuwasogezea wagonjwa huduma karibu na kwa gharama nafuu tofauti na ambavyo wangeifuata huko mkoani ama kwenye hosptali nyingine za rufaa.
Mkuu wa msafara wa madaktari hao ambaye ni Daktari bingwa mifupa Elias Godfley , amesema ndani ya siku tatu upande wa idara ya mifupa wamefanya upasuaji kwa wagonjwa 150.
"Wagonjwa wametoka maeneo mbalimbali ikiwemo Rorya hivyo mwitikio ni mkubwa. Tunawaomba wagonjwa waendelee kujitokeza kwani huduma itahitimishwa machi 1, 2025.
Deus Kituri ni mgonjwa aliyepata ajali na kuvunjika mguu miaka kadhaa iliyopita akatibiwa lakini mguu huo unamsumbua. Amefika hosptalini hapo kuchunguzwa.
"Huu mguu unanisumbua tangu 2018 , ,nimefika hapa nimechukuliwa vipimo kwa ajiri ya uchunguzi zaidi na sasa nipo nasubiru majibu, huduma ni nzuri, amesema Deus.
Dickson magiga mtoto wa miaka 12 aliyevunjika mkono na kupinda naye alikuwa kwenye foleni akisubiria huduma ambapo baba yake mzazi
Maginga Mete amesema wametokea Kijiji cha kikomori kata ya Susuni.
Post a Comment