WACHUNGAJI SDA WALAANI MUUMINI KUJINYONGA
Na Helena Magabe,Tarime
WACHUNGAJI wa Kanisa la Waadventist Wasabato Tarime wamelaani vikali kitendo cha muunini wao Marehemu John Muhabe kujiondoa uhai wake kwa kujinyonga jambo ambalo wamesema ni makosa kisheria na kwa Mungu pia kwani kifo cha kujinyonga sio mpango wa Mungu.
Mchungaji Julius Machumu wa Waadevesti Wasabato (SDA) mtaa wa Majengo wenye makanisa manne likiwemo la mtaa wa Tagota akizungumza wakati wa mazishi ya Marehemu John Februari, 02, 2025, mtaa wa Kogete , amesikitika kumpoteza muumini wake na kusema kuwa sio kwamba marehemu hakuugua ugonjwa wowote kama ilivyoelezwa kwenye historia yake bali huwenda alikuwa na ugonjwa wa akili.
"Kama mtu anafikia hatua ya kujiua huyo anakuwa ameugua ugonjwa wa akili ndio maana alijinyonga ,maana akili yake ilichoka na akili ikichoka inalipua na mtu yeyote anaweza kuugua akili na akafanya maamuzi vinginevyo" amesema.
Mchungaji Issack Gama wa Muderspach Memorial Adventist Primary School , amesema kujinyonga sio kifo cha mpango wa Mungu ni kosa kwa Mungu na kisheria.
Mchungaji Issack Gama wa Muderspach Memorial Adventist Primary School akizungumza wakati wa mazishi.
" Pia mtu anapojinyonga anaacha familia njia panda na anaiachia majibu ya sintofahamu, kataka tamaduni zetu za kiafrika wazazi wanapofanya mambo kama hayo yanaumiza kizazi .
" Yaani mzazi kama huyu mwenye miaka zaidi ya 50 anajinyongaje? anakufaje?anaacha hamaki kiasi gani? watanzania wenzangu popote pale mlipo nawomba msifanye matukio kama haya hayana afya kwa Taifa na kwa kanisa " amesema Gama.
Rhobi Charles Mwanachama wa umoja wa mafundi cherehani soko la Rebu Tarime amesema Marehemu John Muhabe maarufu kwa jina la utani mbili mbili alikuwa fundi wao wa kutengeneza cherehani pindi zilipoharibika na alikuwa mvumilivu hata pale walipokuwa hawana pesa , na kwamba pengo lake halina wakuliziba.
" Mbili mbili siku ya jumatano alikuwa hana raha tukamwuliza mheshimiwa mbona leo huna raha hadi uso umekonda? Sisi tulikuwa tunaumwa akatujibu nyinyi mnaumwa na mimi naumwa.
" Alhamisi tukapigiwa simu amejinyonga, tunasikitika sana alikuwa mwanachama mwenzetu hata cherehani ikiharibika unamwita anakutengenezea hata kama huna hela kumpoteza hata pengo lake sijui nani ataliziba"amesema Rhobi.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kogete Alphaxad James Keroma Maginga, amesema Marehemu John Muhabe alikuwa mtu mwenye upendo kwa jamii yake na hivyo wadau mbali mbali wamempigia simu wakiomba siku ya mazishi isogezwe ili washiriki mazishi lakini haikuweza kuwezekana kwani Familia ilishapanga siku ya mazishi .
Samweli John Muhabe ni kijana mkubwa wa marehemu John Muhabe amesema baba yao alikuwa baba mwema ambaye hakuwa na matatizo yoyote alikuwa anaipenda familia yake hakuwa aliyewapenda watu wote.
Marehemu John Muhabe alizaliwa 1961 alijiunga kwenye kanisa la Waadevesti wasabato Tagota 1996 baada ya kuhama toka mtaa wa Bugosi na kuhamia mtaa wa Kogete.
Ameshika nyadhifa mbalimbali za kitume katika kanisa hilo lakini tangu mwaka 2023 alirudi nyuma jitihada za viongozi wa kanisa,ndugu na jamaa na marafiki kumrudisha kanisani hazikufanikiwa hadi mauti inamkuta Januari 30,2025 na kuzikwa Februari, 2, 2025.
Waombolezaji wakiwa msibani
Kwaya ya Waadevesti Wasabato,kanisa la Kogete mtaa wa Tagota
Post a Comment