HEADER AD

HEADER AD

MFAHAMU MWENYEKITI WA ZAMANI WA IEBC WAFULA CHEBUKATI

 

Wafula Chebukati Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi  nchini Kenya(IEBC)

Chanzo cha picha

Maelezo ya picha,Wafula Chebukati Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya(IEBC)
  • Autho

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC Wafula Chebukati amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Kaka yake Daniel Chebukati amethibitisha kufariki kwake akiwa na miaka 63. Bosi huyo wa zamani wa IEBC alikuwa amelazwa hospitalini akipokea matibabu kwa wiki nzima.

Chebukati alihudumu kama mwenyekiti wa Tume ya IEBC kwa miaka sita kuanzia Januari 2017 hadi Januari 2023. Katika kipindi cha utumishi wake, alisimamia chaguzi tatu muhimu nchini Kenya: Uchaguzi Mkuu wa Kenya wa 2017, Uchaguzi wa Marudio wa Rais wa Kenya wa Oktoba 2017, na Uchaguzi Mkuu wa Kenya wa 2022.

Wafula Chebukati ,mwanasheria ndiye mwenyekiti wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) inayohusika na mchakato mzima wa uchaguzi nchini Kenya.

Chebukati aligonga vichwa vya habari baada ya uchaguzi mkuu wa 2022 alipomtangaza William Ruto kama mshindi wa uchaguzi wa urais . Rais Ruto alimtaja Chebukati kama 'shujaa'.

Bwana Chebukati mwenye umri wa miaka 60, alikula kiapo cha kuongoza tume hiyo kwa mara ya kwanza mtarehe 20 January 20, 2017, alipomrithi mtangulizi wake Issack Hassan.

'Mwanasheria asiyetetereka'

Wafula Chebukati

Chanzo cha picha

Maelezo ya picha,Wafula Chebukati, Mwenyekiti wa IEBC ni mtu mwenye 'haiba ya upole', lakini hakuwa mtu aliyetetereka katika maamuzi ya kazi yake

Marehemu Wafula Chebukati alikuwa akiongea kwa sauti ya upole na utaratibu, lakini kwa wanaomfahamu si mtu mwenye kutafuna maneno na mara nyingi alichokiongea ndicho alichokimaanisha .

Alinusurika na majaribio kadhaa ya kutaka kumng'oa kwenye wadhifa wake hususan baada ya Mahakama ya juu zaidi chini ya uongozi wa Jaji Mkuu David Maraga kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2017.

Tume aliyoiongoza ilishutumiwa zaidi na upinzani kwa udanganyifu katika mchakato mzima wa upigaji kura na ukusanyaji wa matokeo. Hatahivyo Bw Chebukati aliapa kuwa kamwe hatojizulu kutoka wadhifa wake akijitetea mara kwa mara kuwa utendaji wake unafuata misingi ya katiba.

Wafula chebukati

Chanzo cha pic

Licha ya kujiuzulu kwa makamishna watatu wa tume hiyo mwaka wa 2018 baadhi walitegemea kuwa angejiuzulu pia, hususan kutokana na wito wa kumtaka aondoke madarakani. Hatahivyo Bw Wafula Chebukati aliapa kuendelea kuongoza tume hiyo, akiwashtumu makamishna hao waliojiuzulu kwa kushindwa kupokea maoni tofauti.

Mwenyekiti huyo wa IEBC alisema makamishna hao watatu hawakujiuzulu kwa kutokana na kanuni za kiutendaji , bali "sababu halisi ya kujiuzulu kwao ni uamuazi wa kikao wa kumuwajibisha Afisa mkuu mtendaji wa tume ya uchaguzi (Ezra Chiloba) ."

Bw Chebukati pamoja na Bw William Ruto

Chanzo cha picha

Maelezo ya picha,Rais, William Samoei Ruto aliyekuwa mgombea wa chama cha United Democratic Alliance -UDA (kushoto) akiwasilisha nyaraka za uteuzi wake kwa ajili ya kuidhinishwa na Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati, enzi za uhai wake

Uamuzi huu ulifuatiwa na hatua ya mgombea wa Muungano wa upinzani Bw Raila Odinga wa kususia kurudiwa kwa uchaguzi, ambapo aliikataa bodi ya utawala ya tume ya IEBC ya kurekebisha mapungufu yaliyotambuliwa na Mahakama Kuu, jambo lililoibua uwezekano wa msukosuko nchini.

Bw Wafula Wanyonyi Chebukati alishuhudia Bw Odinga akichukua jukumu la Tume anayoiongoza na kujiapisha binafsi kama ' Rais wa Watu', baada ya Rais wa wakati huo Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kushinda bila kupingwa katika uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 2017, hatua iliyoashiria kuwa mzozo wa kisiasa ungekuwa wa muda mrefu.

Mzozo huo ulisitishwa tu wakati Bw Kenyatta na Bw Odinga walipoamua kuafikiana kupitia mkataba maarufu wa 'Handshake' mwezi Machi mwaka huo.

Wafula chebukati na Raila Odinga

Chanzo cha picha,

Maelezo ya picha,Raila Odinga (kulia), mgombea wa urais wa Muungano wa Azimio la Umoja, baada ya kuidhinishwa na tume ya IEBC kugombea kiti cha urais, akipewa cheti na Mwenyekiti wa IEBC, Bw Wafula Chebukati.

Wafula Wanyonyi Chebukati ni nani ?

Wafula Chebukati alizaliwa tarehe 22 Disemba , 1961 katika kaunti ya Bungoma magharibi mwa Kenya.

Alipata elimu yake ya sekondari katika chule ya St. Peters Mumias, Bokoli na pia katika shule ya Lenana High na baada ya hapo alijiunga na Chuo kikuu cha Nairobi ambako alisomea sheria. Alihitimu katika Chuo kikuu cha Nairobi na kupata shahada ya sheria mwaka 1985 na baadaye akajiunga na Chuo cha sheria cha Kenya na kusajiliwa kama wakili mwaka 1986.

Bw Wafula Chebukati pia ana shahada ya uzamili ya utawala wa biashara aliyoisomea katika Chuo kikuu cha Kilimo na masomo ya Kiufundi cha Jomo Kenyatta (JKUAT). Wafula Chebukati amebobea katika nyanja ya sheria ya biashara ya kimataifa, sheria ya uwekezaji, sheria ya ushirika, na sheria kuhusu utawala na mazingira.

Chebukati

Chanzo cha picha,

Ni muasisi mwenza wa kampuni ya mawakili ya Cootow & Associates Advocates, ambayo ni kampuni ya sheria inayotoa huduma za kisheria kuanzia za usafirishaji wa majini, usafiri wa ndege, suluhu mbadala ya mizozo (ADR) bima kwa benki na sheria za kibiashara.

Mwaka 2007, Bw Chebukati alijitosa kuwania ubunge wa wa eneo la Saboti kupitia chama cha kisiasa cha ODM lakini alishindwa na Waziri wa sasa wa Ulinzi Eugene Wamalwa ambaye wakati huo aligombea kiti hicho kwa tiketi ya chama cha -PNU (Party of National Unity).

Chebukati alijiuzulu kutoka chama cha ODM kabla ya kuomba kazi katika tume ya hiyo ya uchaguzi.

Chanzo : BBC

No comments