HEADER AD

HEADER AD

MKOA WA MARA WATAKIWA KUONGEZA THAMANI YA MAZAO

>> Naibu Waziri wa viwanda na biashara asema mkoa  huo ukiongeza thamani ya mazao utawavutia wawekezaji sekta ya mifugo na uvuvi

Na Ada Ouko, Musoma

NAIBU waziri wa viwanda na biashara Exaud Kigahe, ameutaka mkoa wa Mara kuweka mkakati wa kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa kutokana na sekta ya mifugo na uvuvi ili kuwavutia wawekezaji.

Amesema hayo januari 25 mwaka huu 2025 kabla ya kuanza ziara yake ya siku mbili ya kikazi mkoani ni humo punde alipowasiri katika ofisi ya mkuu wa mkoa huo kwa ajili ya salamu na kusaini kitabu cha wageni, ambapo amesema moja ya utekelezaji wa maelekezo ya Raisi Samia Hassan kuwa ni kumsaidia muwekezaji kufanikiwa.

      Naibu  waziri wa viwanda na biashara Exaud Kigahe akizungumza 

"Bado naiona Mara ina fursa mwenye maeneo mengi ikiwemo kuiweka kuwa kinara kwenye sekta ya uongezaji thamani katika uzalishaji wa mazao yanayotokana na mifugo na uvuvi nadhani hilo ndio lengo kubwa tuone namna gani tunaifufua tena Mara" amesema Kigahe.

Amesema kupitia kuchakata na kuongeza thamani katika sekta hiyo ya kimkakati ya mifugo na uvuvi itasaidia kuongeza ushindani wa kibiashara kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi hali itakayopelekea kukua kwa uchumi wa mkoa huo na Taifa kwa ujumla.

Kufuatia kuwepo kwa changamoto ya upungufu wa sukari na mafuta ya kula, amesema mkoa huo pia unapaswa kujikita katika kilimo cha biashara kwenye miwa na uzalishaji wa zao la kahawa jambo ambalo alisema kama wizara husika italishughulikia.

Naye mkuu wa mkoa huo, Kanali Evans Mtambi amesema kwa sasa mkoa unatekeleza kampeni maalumu ya kukabiliana na wavuvi haramu ili kulinda mazalia ya samaki na viumba hai wengine wanaoishi kwenye ziwa viktoria mkoani hapa.

         Mkuu wa mkoa wa Mara , Kanali Evans Mtambi

"Tusaidie kuvitazama viwanda vyetu ambavyo kwa namna moja au nyingine vilishindwa kukidhi vigezo vya ukezaji vikachukulia wa na serikali ikiwa ni kwa kuvibinafsisha ili tuweze kupata wawekezaji na hatimaye vianze uzalishaji" amesema.

Awali Kaimu Afisa biashara wa Mkoa huo Gambaless Timotheo amesema mkoa huo una viwanda vitatu vya kuchakata kahawa ambavyo vipo wilayani Tarime alivitaja kuwa ni Mara Coffee, Northern Highlight,  na Muccu na kwamba vinafanya kazi hali inayopelekea zao hilo kufanya vizuri mkoani humo.






No comments