HEADER AD

HEADER AD

EWURA YAWATAKA WAKAZI KANDA YA ZIWA KUWAEPUKA VISHOKA

 


Na Alodia Dominick,Bukob,

WAKAZI wa kanda ya ziwa wameaswa kutumia mafundi wa kufunga mifumo ya umeme kwenye majengo ambao wana leseni ili kuepukana na vishoko ambao ufanyaji kazi za kufunga mifumo ya umeme hauwaruhusu kisheria.

 Lai hiyo imetolewa na meneja wa kanda ya ziwa wa mamlaka ya udhibiti wa nishati  na maji EWURA Goerge Mhina wakati akitoa mafunzo kwa mafundi wa kufunga umeme majengo mkoa wa Kagera, mafunzo yaliyofanyika manispaa ya Bukoba.

  Washiriki katika mafunzo

Mhina ametaja lengo la kukutana na mafundi hao kuwa ni kuwakumbusha umuhimu wa taaluma yao maana taaaluma yao ni muhimu sana katika kufanya kazi kwa sababu ili Tanesco waweze kuingiza umeme kwenye jengo lolote lazima kazi hiyo iwe imepitia kwa hao mafundi.

"Kwa siku za karibuni tumekuwa tukishuhudia majanga mbalimbali ya kuungua kwa majengo ambapo wakati mwingine ni rahisi kwa mtu kusema chanzo ni hitlafu ya umeme wa TANESCO lakini uchunguzi unapofanyika tunakuta moto ule ulisababishwa na kazi mbovu au vifaa vilivyotumika vilikuwa duni na kusababisha moto kutokea" amesema Mhina

Amesema, wamewakumbusha mafundi  kwamba wana jukumu kubwa katika kazi zao ikiwa ni kuzingatia sheria, lakini kuifanya kazi hiyo kwa weledi kuepuka majanga ya moto ambayo yanapelekea kupotea kwa mali na wakati mwingine vifo.

Ameongeza kuwa mafundi hao wanaongozwa na sheria ya umeme pamoja na kanuni mbalimbali ambazo zimetengenezwa na EWURA na mtu yeyote haruhusiwi kufanya kazi ya kuweka mifumo ya umeme kwenye majengo pasipokuwa na leseni kutoka EWURA.

       Meneja wa Ewura kanda ya ziwa George Mhina

"Sisi EWURA ndo tunatoa leseni kulingana na weledi wa mtu na yapo madaraja mbalimbali tulikuwa tumewasiditiza kwa wale ambao  hawana leseni waje kwetu watafute leseni lakini pia wafanye kazi kwa weledi kwa sababu tunapoelekea sada hivi pale ambapo jengo litaonekana limeungua tunatafuta kama chanzo siyo umeme wa TANESCO ni kazi mbaya iliyofanywa na mkandarasi" amesema Mhina 

Ameongeza kuwa, itafika mahali mkandarasi atapaswa kuwajibika kisheria kwa kushitakiwa yeye mwenyewe kutokana na hasara aliyosababisha ambayo imeleta majanga.

Amesema miongoni mwa kazi za EWURA ni kushughulikia malalamiko katika sekta za umeme, mafuta, gesi asilia pamoja na maji.

Aidha alitaja idadi ya mafundi umeme kwa Tanzania kuwa wako zaidi ya 6,000  ambao wana leseni, kwa kanda ya ziwa kuwa idadi yao ni 497 na mkoa wa Kagera mafundi 147.

 Ofisa mahusiano huduma kwa wateja Tanesco mkoa wa Kagera Lilian Mungai ameeleza jitihada za shirika hilo katika kuhakikisha wanaondoa  tatizo la vishoka,matapeli,wakandarasi na mafundi wasio na leseni  kwa kuanzisha utaratibu mpya unaitwa nikonekti.

 Amesema, utaratibu huo una uwazi mkubwa  ambao  utaondoa  madhara kwa wananchi ambapo kila mtu ambaye anahitaji kufungiwa umeme anaweza kufanya maombi yake kupitia simu yake ya mkononi au kompyuta kuingia katika tovuti ya nikonekti.

"Vishoka wamekuwa wakitumia jina la Tanesco wakiwalaghai wateja wetu kuwa kuna gharama za kufunga waya na kufanya michoro ambayo sisi binafsi hatuhusiki  hivyo,tunatoa wito kama wananchi watashindwa kufanya maombi kupitia simu za mkononi basi wafike ofisini au wanaweza kupiga simu kupitia namba ya huduma kwa wateja ili waweze kupata huduma stahiki "ameeleza Mungai.

Rwagaya Buberwa ambaye ni mkandarasi wa umeme mwenye leseni ambaye anahusika na ufungaji wa umeme katika majengo amesema shida au changamoto ya kufungiwa umeme alafu nyumba ikapata itilafu na kuungua inatokana na watoa huduma zaidi ya mmoja ikiwemo wale ambao hawajathibitishwa na Ewura na kupata leseni .

Aidha amesema, Kubwa ni elimu itolewe kwa wananchi kupitia Ewura na Tanesco kwa wakandarasi kwa kushirikiana na mamlaka husika wahakikishe wanatoa elimu, kwa kuelekeza,kusimamia na kudhibiti na kusuka mifumo ambayo inaendana na viwango vinavyostahili hiyo  itaondoa mianya ya vishoka  kujipenyeza na kuwarubuni wananchi.


No comments