Home
/
HABARI MCHANGANYIKO
/
MRATIBU KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA AWASHAURI WANANCHI KUANDIKA WOSIA
MRATIBU KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA AWASHAURI WANANCHI KUANDIKA WOSIA
Na Gustaphu Haule, Pwani
MRATIBU wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia katika Halmashauri ya Wilaya Kibaha Egidy Mkolwe,ametoa ushauri kwa wananchi wa Kijiji cha Kwala Kata ya Kwala kuhakikisha wanaandika wosia wa mali zao.
Mkolwe ambaye pia ni Wakili wa Serikali ametoa ushauri huo Februari 28 ,2025 wakati akizungumza na wanaKijiji hao katika mkutano maalum wa kutoa elimu ya sheria uliofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya Serikali ya Kijiji hicho .
Mkolwe amesema kuwa kuandika wosia ni muhimu kwakuwa unasaidia kuondoa migogoro katika familia kipindi ambacho mmiliki wa mali husika anapofariki.
Mratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia ambaye pia ni Wakili wa Serikali Egidy Mkolwe akitoa elimu ya namna ya kutatua migogoro ya ardhi kwa Wananchi wa Kijiji cha Kwala Kata ya Kwala katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha .
Amesema familia nyingi huwa zinakumbwa na migogoro mpaka kufikia watu kuuana kwakuwa tu marehemu hakuacha wosia huku akisema kwasasa lazima wabadilike na waendane na wakati uliopo.
Mkolwe amesema mtu akitaka kuandika wosia lazima huwe wa siri kwasababu watu wakijua nani amepewa wosia wa mali hizo ni wazi kuwa familia inaweza kusambaratika na hivyo kujengeana chuki.
Mkolwe amesema wosia mzuri unapaswa kutengenezwa na Wakili ambapo amesema kupitia kwa Wakili itakuwa njia sahihi na yenye msaada hususani kwa wale ambao wana watoto wengi.
Wananchi wa Kijiji cha Kwala katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wakiwa katika mkutano wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia uliofanyika Februari 28 Kijijini hapo.
"Nashauri wananchi waandike wosia mapema na wosia huo huwe wa maandishi na sio maneno,na kama mtu anatoa wosia wa maneno ni lazima hapate mashahidi wengi,"amesema Mkolwe
Amesema kuwa kutokana na changamoto zinazojitokeza katika jamii hususani katika masuala ya Mirathi Rais wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan akaona alete kampeni ya msaada wa kisheria kwa ajili ya kusaidia Wananchi wake.
Baadhi ya wataalam wanaotekeleza Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha akiwemo Mkuu wa dawati la Jinsia kutoka Wilaya ya Kipolisi Mlandizi Inspekta Tumaini Ulimboka wa pili kushoto mwenye T-shirt nyekunde wakitoa msaada wa kisheria
"Kampeni hii ya msaada wa kisheria imeanzishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan lengo ni kutaka kuona watu wake wa chini wanasaidiwa katika masuala mbalimbali yanayohitaji msaada wa kisheria ikiwemo migogoro ya ardhi,miradhi,Taraka na Ndoa,"amesema
Timu hiyo ikiwa katika Kata ya Kwala imetoa elimu ya ukatili dhidi ya watoto na wanawake, haki na wajibu wa mtoto pamoja na kuhamasisha watoto kutoa taarifa za ukatili wanaofanyiwa na Walimu, Wazazi, Ndugu,jamaa na marafiki katika Shule tatu za msingi na Shule moja ya
Sekondari.
Mkazi wa Kijiji cha Kwala Tausi Msemakweli, amesema kuwa elimu ya msaada wa kisheria imekuwa na faida kubwa kwake ambapo ameomba elimu hiyo hiwe endelevu angalau mara tatu kwa mwaka.
Post a Comment